Ludwina Godfrey, Michael
Nkwabi, Pascalina Slyvester, Lameck Misiwa, Deogratius Lazaro
Umoja, Upendo, Furaha,
Amani ni miongoni mwa mambo ambayo huweza kufanikisha mambo mengi katika kundi
la watu au jamii husika.
Wanariadha wa klabu ya
riadha ya Holili Youth (HYAC) iliyopo katika kijiji cha Holili wilayani Rombo
mkoani Kilimanjaro wamejaliwa kuwa na mambo hayo.
Wakati wote hufurahi,
kila mmoja akiwa na amani na mwenzake hali ambayo imekuwa ikifanikisha sana
utendaji wa klabu hiyo.
Ikumbukwe kwamba HYAC
imejielekeza zaidi katika kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji vya vijana wanaopenda
mchezo wa riadha.
Kwa miongo kadhaa sasa
medani ya riadha nchini imepoteza mwelekeo hali ambayo imekuwa ikishusha mwamko
wa vijana.
Hii imetokana na ukweli
kwamba serikali imeshindwa kuelekeza nguvu zake katika shule za msingi na sekondari
ambako kuna vijana chipukizi wanaoweza kuiletea sifa nchi ya Tanzania katika
medani hii adhimu.
Hata hivyo licha ya
kusuasua huko bado jitihada za mmoja mmoja zinaendelea ikiwemo vilabu
mbalimbali nchini kuwa na ari ya kuinua mchezo husika.
Holili Youth Athletics
Club (HYAC) ni miongoni mwa wadau muhimu wa mchezo wa riadha licha ya ukosefu
wa wafadhili katika maeneo mbalimbali.
Imejitahidi kuweka
kambi ambako nyota wa mchezo huo huendelea kufanya mazoezi ya pamoja.
Lameck Misiwa, Michael
Nkwabi,Furaha Sabaya, Deogratius Lazaro na Ludwina Godfrey
Deogratius Lazaro
Furaha Sabaya na Michael
Nkwabi
Furaha Sabaya
Rehema, HYAC matron in
the camp
Lameck Misiwa
Ludwina Godfrey
Michael Nkwabi
Pascalina Slyvester na
Adelina Audax
Pascalina Slyvester,
Adelina Audax na Neema Mathias
No comments:
Post a Comment