Toleo
la Mei 2014
Yaliyomo
- UTANGULIZI
- HOLILI YOUTH ATHLETICS CLUB
- UNAWAKUMBUKA?
- AFYA NA RIADHA
- SURPRISE RIO!
- B’E
- TO THE BEST
- BIOGRAPHY CHAMBER
Kona
ya PRO-ni kijarida kidogo cha kwenye mtandao ambacho hutolewa kila
,mwezi na Holili Youth Athletics Club(HYAC). Kimekusanya masuala kadhaa
yanayohusu mchezo wa riadha, fuatana nasi hadi mwisho kwa yale tuliyokuandalia
kwa mwezi Mei mwaka huu.
Itakumbukwa kwamba riadha ni mchezo unaopendwa na watu
wengi ulimwenguni kwani ndio mchezo mama wa michezo mbalimbali ulimwengu. Umekuwa ukihusisha mwili wa
binadamu kwa kiasi kikubwa. Pia mchezo huu umekuwa ukihusisha mtu mmoja mmoja katika ushindani
wake ukiachia relay races.
Riadha (Athletics) michezo mbalimbali kama kukimbia (running), kuruka (jumping),
kurusha (throwing) na kutembea (walking). Hata hivyo kuna aina tatu za
riadha ambazo ni Track and Field, Road
Running, Cross country na Race Walking.
Domician
Genandi
Mkurugenzi
Mtendaji
Holili Youth Athletics Club (HYAC).
Domician Rwezaura Genandi ni
miongoni mwa mamia ya waanzilishi na wamiliki wa klabu za riadha hapa
ulimwenguni wenye shauku ya kuinua mchezo huo ujulikane zaidi, kila pembe ya
dunia.Mwanzilishi huyu ndiye pekee mwenye klabu yenye malengo ya kuwainua
wanariadha nchini Tanzania hususani vijana wanaochipukia katika mchezo huo.
HYAC inapatikana katika Kijiji
cha Holili kilichopo mpakani mwa Tanzania na Kenya katika wilaya ya Rombo ikiwa
ni kilometa 36 kutoka Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro. Itakumbukwa kwamba Holili Youth
Athletics Club (HYAC) ilianza kujihusisha na masuala ya riadha mwaka 2010 na
kusajiliwa rasmi Oktoba 25, 2011. Mwaka 2011 ilijipatia usajili
wake kutoka Baraza la Michezo nchini Tanzania (BMT) Na. 9833.
Holili ipo katika miteremko ya
Mlima mahiri ulimwenguni wa Kilimanjaro na kambi ya mafunzo kwa wachezaji wake
ipo katika Mjini wa Tarakea mpakani mwa Tanzania na Kenya.
Holili Youth Athletics Club
(HYAC) inajitahidi kufanya yafuatayo, ikiwa na malengo ya kuuinua vipaji vya
wanariadha nchini na mchezo wenyewe kwa ujumla.
Wanariadha wa HYAC, wakijiandaa
kukimbia mita 5,000, Kili Marathon 2014 iliyofanyika mjini Moshi.
|
•
Falsafa
yetu ni kufanya kazi kwa bidii na kujitoa, Falsafa hiyo inaongozwa na kauli
mbiu ya “ Michezo huwaweka watu pamoja, Njoo Ujiunge nasi”(Sports brings people together come and join us).
•
Holili
Youth Athletics Club inajitoa kwa muda, hali na mali kwa ajili ya kuifanya
klabu isonge mbele kwa matokeo mazuri. Hivyo inatarajia mwanariadha ataongeza
bidii katika mazoezi ili kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali.
•
HYAC
ina wafanyakazi ambao sharti wawe waaminifu kwelikweli, ambapo wanatarajia
kuona wanariadha wanapofanya vizuri ndio furaha kwao kwani malengo ya
kuinuamchezo wa riadha yanafikiwa.
•
Hata
hivyo klabu hii, pekee ya riadha nchini Tanzania yenye ari na hamasa ya kuinua
mchezo wa riadha inaendelea na juhudi za kutafuta ushauri kutoka kwa wanariadha
waliowahi kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa kwenye maeneo ambao
hawana ufahamu nayo kwa malengo kwamba mwanariadha wa HYAC aweze kupata nafasi
ya kusonga mbele.
Leo,
katika kipengele hiki ninakuletea Wanariadha watano waliovunja rekodi kabla ya
mwaka 2005 katika mbio za kilometa 42 (Full Marathon).
NA.
|
JINA
|
NCHI
|
MUDA
|
MWAKA
|
MBIO
|
1
|
Paul Tergat
|
KENYA
|
2:04.55
|
2003
|
BERLIN
|
2
|
Khalid Khanouchi
|
MOROCCO
|
2:05.38
|
2002
|
LONDON
|
3
|
Khalid Khanouchi
|
MOROCCO
|
2:05.42
|
1999
|
CHICAGO
|
4
|
Ronaldo da Costa
|
BRAZIL
|
2:06.05
|
1998
|
BERLIN
|
5
|
Belayneh Dinsamo
|
ETHIOPIA
|
2:06.50
|
1988
|
ROTTERDAM
|
MWILI
WA BINADAMU
Mwili wa binadamu ni mashine
inayoishi na ili kuufahamu vizuri ni muhimu kuusoma jinsi ulivyoundwa, kwa
kufanya hivyo itasaidia kukuza mchezo wenyewe.
Makocha wengi wamekuwa
wakishindwa kuwafundisha wachezaji wao vipaji, kutokana na uelewa finyu wa
namna mwili wa binadamu ulivyo.
Wakati mwingine mchezaji
anaweza kutojisikia vizuri kutokana na masuala mbalimbali msichana ama mvulana huku
mwalimu akimtaka kuendelea kukimbia wakati viungo vya mwili vimegoma.
Wakimbiaji (athletes) wanaweza
kuwa na maumbo na maumbile tofauti, rangi za ngozi zao zikawa tofauti lakini
suala la mwili kufanya kazi hufanyika bila kujali hayo kwani wao ni watu
walioumbwa kwa mifupa na mishipa.
Huhitaji mpaka uwe daktari
kuujua mwili wa binadamu kwa ajili ya mchezo wa riadha, hivyo unaweza kuelewa
kupitia “Kona ya PRO” namna gani mwili wa binadamu anavyoweza kufanya kazi.
Mwili wa binadamu umeundwa na
mambao yafuatayo:
- Seli
- Mifupa
- Mishipa
- Neva za Mawasiliano
SELI
(Cells)
Viumbe hai vyote vinandwa na
seli moja au zaidi. Mwili wa binadamu unaundwa na mamilioni ya seli ndogondogo
zinazoishi.
Seli ndizo zinaunda ngozi yetu,
mifupa yetu, mishipa, ubongo na vingine vingi katika miili yetu.
Hivyo kila tunachokifanya
kinahusisha mamilioni ya seli ndogondogo zinazoishi zenye maumbo na ujazo
tofauti ambapo hufanya kazi pamoja kufikia malengo.
Kila aina seli hufanya kazi
mbalimbali, ambapo huchukua ujumbe kutoka sehemu moja kwenda nyingine, huchukua
kemikali ambazo hubeba hewa ya oksjeni, seli hizo hufanya mwili usimame pia
husababisha mwili utembee.
Kila seli hufanya kazi yake,
lakini kwa ujumla wake huishi, hukua na hatimaye kufa na seli nyingine huchukua
nafasi na kuendelea na jukumu la kuufanya mwili ufanye kazi yake.
SKELETON
Binadamu, kama walivyo wanyama
wakubwa, wana skeleton katika miili yao. Skeleton ni mfumo wa mifupa na vitu
vingine vinavyoupa kuutwa mfupa.
Skeleton hufanya kazi tatu
ambazo ni
- Support
Skeleton
inafanya kazi kama ambavyo wajenzi huweka msingi ili nyumba isimame. Bila
skeleton, mwili wa binadamu usingekuwa na umbo lolote la kueleweka.
- Protection
Skeleton
inaweka ulinzi wa viungo ambavyo ni
laini vinavyoweza kuathirika kwa haraka, kwa mfano moyo ubongo unalindwa na
fuvu ambalo ni mkusanyiko wa mifupa.
- Movement
Skeleton
husababisha mwendo baada ya misuli kuunganika na mfupa. Hiyo misuli
iliyounganika kwenye mfupa ndio inafanya jointi zifanye kazi. Katika hilo skeleton
huweka balance (uwiano sawa) ndipo mwili unaweza kutembea.
Katika masuala ya riadha ni
muhimu sana kuelewa namna ambavyo mwili
wa binadamu unaweza kufanya kazi, ili kuleta matokeo chanya kwa mchezaji
husika.
Itaendelea
toleo lijalo…
Kwa mara ya kwanza, “SURPRISE RIO!” ni kipengele
kitakachokuwa kikikuletea matukio ya kushangaza, kuchekesha, kuhuzunisha na
wakati mwingine kukupanua ufahamu.
Leo, nitawaangazia wafuatao:
Mwanadada huyo katika mbio za
Sokoine Min Marathon Kilometa 2 ambaye hakufahamika jina mara moja.
Huyo ni miongoni mwa
waliokimbia kilometa mbili lakini kabla ya kuanza Kona ya Pro iliyasikia maneno ya watani wa mwanadada huyo kuwa ,
ingekuwa vema aandike kwanza wosia.
Maneno hayo yalikuwa na maana
gani? Kumbe walijua wazi kuwa angechoka sana, ndivyo ilivyokuwa, alipokuwa
akimaliza mbio hizo Maafisa walimpokea akiwa hoi bin taabani na kumhudumia.
Pili, wanariadha vipaji
waliokosa matunzo, Kona ya Pro
ilishuhudia jinsi ambavyo wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari wa Kijiji
alichozaliwa Hayati Edward Moringe Sokoine wakichuana katika kilometa 2,
wasichana kwa wavulana ilikuwa patashika nguo kuchanika.
B’E ni kifupisho cha maneno
yafuatayo, “BIG EVENT” . Leo katika kipengele hiki tunakuletea tukio la
kimichezo lililokuwa na mvuto kwa mwezi Aprili mwaka huu.
Sokoine
Min Marathon 2014
Sokoine Min Marathon 2014
ilifanyika kwa mara ya pili mfululizo kwa ajili ya kuadhimisha miaka 30 ya kifo
cha Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Edward
Moringe Sokoine.
Hayati Sokoine alifariki kwa
ajali Aprili 12, 1984 mkoani Dodoma. Aprili 12, 2014 ilikuwa ni
miaka 30 tangu kutoweka duniani kwa kiongozi huyo ambaye anatajwa kuwa
mwadilifu na mzalendo.
Maadhimisho hayo yaliwaleta
karibu viongozi mbalimbali wa kisiasa ambao walimiminika akiwemo Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Jakaya Kikwete, Rais
wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Benjamin Mkapa na Waziri Mkuu
Aliyejiuzulu wadhifa huo Mheshimiwa Edward Lowassa.
Maalim Seif Sharrif Hamad
Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar alihudhuria
maadhimisho hayo yaliyopambwa na gwaride kutoka majeshi ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania.
Michezo mbalimbali ya Riadha
ilifanyika ikiwemo kukimbia mingine ni Kurusha Mkuki na kuruka.
Holili Youth Athletics Club (HYAC)
ilichomoza kwa kishindo katika Sokoine Min Marathon kwa kilometa 2 na kilometa
10.
Adelina Audax, Neema Mathias na
Lidiuna Godfrey walichukua nafasi tatu za juu baada ya kuwashinda wanariadha wa
kike waliokimbia kilometa 2.
Alphonce Felix alichomoza
nafasi ya pili kilometa 10 akiiwakilisha Holili Youth Athletics Club (HYAC)
akikimbia kwa muda wa dakika 34:45.39 akiachwa na Fabian Joseph kwa sekunde 16
(34:28.04).
Nafasi ya tatu ilishikwa na
Bingwa wa Sokoine Min Marathon 2013, Dickson Marwa (HYAC) akikimbia kwa dakika
34:57.47
Kwa wanawake kilometa 10
mwanadada Jackline Sakilu, Bingwa Kili Marathon 2014 kilometa 21, alitwaa taji
hilo akiliwakilisha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) akikimbia kwa dakika
40:01.26 akifuatiwa na Nathalia Elisante kutoka mkoani Arusha akitumia muda wa
dakika 40:51.27 na nafasi ya tatu ilinyakuliwa na Failuna Abdi kutoka Winning
Spirit Arusha akifukuza upepo kwa dakika 41:13.54
Kwa upande wa wavulana kilometa
2 Oshun Simon (Nanja Secondary School) alitwaa taji hilo; huku nafasi ya pili
na tatu ikichukuliwa na vijana kutoka Shule ya Sekondari ya Moita ambao ni
Kalei Mereso na Ngoyai Ormeki.
Sabero Naisike wa Shule ya
Sekondari ya Orkeswa alishika nafasi ya nne na nafasi ya tano ilichukuliwa na
Lengarusi Tpasoi wa Shule ya Sekondari Nanja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Holili
Youth Athletics Club, Domician Genandi alisema anafurahi kuona chipukizi
aliowaandaa wanafanya vizuri katika medani ya riadha katika michuano hiyo.
Genandi aliongeza kusema
Sokoine Min Marathon inaweza kuinua vipaji vya riadha kuanzia shule za msingi
hasa ikizingatia kulionekana vipaji vizuri vya mbio hizo, ambavyo vikitafutiwa
mazingira vinaweza kuing’arisha medani ya
riadha nchini.
Hata hivyo alitaka mbio za
Sokoine Min Marathon zitengewe siku yake ili kuleta ladha zaidi hususani kwa
masuala ya kiuchumi watu wa eneo hilo waweze kufanya biashara zao kwa uhuru
hasa ikizingatiwa kwamba “Sokoine Day” hutawaliwa na shughuli nyingi za
kisiasa.
Itakumbukwa kwamba Hayati
Edward Moringe Sokoine alizaliwa Agosti 1, 1938 Kilasho Kijiji cha Emairete
Monduli Juu mkoani Arusha kwa wazazi wake Baba Sokoine Ole Severe na Mama
Napelel Sinyati Noomoyaki.
Sokoine
Min Marathon 2014 Kilometa 2
Kilometa
2, kwa wanafunzi wa Shule za Msingi, Wasichana Nawasa
Kamoyo(Euyati) alishika nafasi ya kwanza akifuatiwa na Patricia Leliel (Mazoezi),
na nafasi ya tatu ikinyakuliwa na Neiyo Simon kutoka Shule ya Msingi Euyati.
Wavulana
waliokimbia kilometa 2 na kushika nafasi tatu za kwanza walikuwa Kibori
Jackson (Monduli Juu), Emmanuel Clakoi (Monduli Juu) na Paulo Leken (Monduli Juu).
Kilometa
10
WANAUME
|
||||
1
|
Fabian Joseph
|
34:28.04
|
WNS
|
|
2
|
Alphonce Felix
|
34:45.39
|
HYAC
|
|
3
|
Dickson Marwa
|
34:57.47
|
HYAC
|
|
4
|
Gabriel Gerald
|
34:59.09
|
WNS
|
|
5
|
Fabian Nelson
|
35:07.20
|
CCP
|
WANAWAKE
|
||||
1
|
Jackline Sakilu
|
40:01.26
|
JWTZ
|
|
2
|
Nathalia Elisante
|
40:51.27
|
ARUSHA
|
|
3
|
Failuna Abdi
|
41:13.54
|
WNS
|
|
4
|
Mary Naali
|
41:25.15
|
AAAC
|
|
5
|
Serina Amosi
|
43:24.70
|
ZANZIBAR
|
|
6
|
Flora Yuda
|
44:52.99
|
JWTZ
|
April
12, 2014; Mwanariadha chipukizi Adelina Audax (HYAC) aliibuka kidedea
katika mbio za kuadhimisha miaka 30 tangu kifo cha Aliyekuwa Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine.
Adelina alitwaa taji la Sokoine
Min Marathon kilometa 2 kwa upande wa wasichana katika ardhi ya Monduli Juu
mkoani Arusha, mahali alipozaliwa Waziri huyo.
Adelina Audax anayetunzwa na
Holili Youth Athletics Club katika kambi ya mazoezi ya klabu hiyo iliyopo
Tarakea wilayani Rombo aliwaongoza wasichana wenzake kutoka klabu hapo Neema
Mathias na Lidiuna Godfrey alishika nafasi ya tatu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete alimkabidhi taji la ushindi mbele ya viongozi
wengi wa kisiasa na kidini waliohudhuria maadhimisho ya kifo cha Waziri Mkuu wa
Zamani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Edward Sokoine.
Hayati Sokoine alifariki dunia
Aprili 12, 1984 kwa ajali ya gari, mkoani Dodoma.
Leo
katika “BIOGRAPHY CHAMBER” tumekueandalia Historia ya Mwanzilishi wa Klabu ya
Riadha ya Holili (HYAC), Domician Genandi.
DOMICIAN
GENANDI NI NANI?
Jina lake ni Domician Genandi
Rwezaura (47), alizaliwa Desemba 29, 1967 katika kijiji cha Kagondo Wilayani
Muleba mkoani Kagera.
Elimu ya Msingi aliipata katika
Shule ya Msingi Kableme kijijini hapo kati ya mwaka 1980-1987. akafanikiwa
kuendelea na masomo ya sekondari kati ya mwaka 1988-1992 (O-level) na 1993-1995
(A-level) katika Seminari ya Kikatoliki ya Uhuru iliyoko mkoani Kilimanjaro.
Kutokana na wito wake wa kuwa
mtumishi wa kanisa la Katoliki (Upadre) aliamua kwenda kusomea masomo ya
Falsafa katika Chuo cha Kanisa hilo kilichopo Nairobi (CUEA-Catholic University
of East Africa) kati ya mwaka 1996-1999, Advanced Diploma of Philosophy.
Aliachana na masuala ya wito katika kanisa hilo baada ya kumaliza mafunzo hayo
ya miaka mitatu (3) mara baada ya kugundua anatakiwa aitumikie jamii akiwa
ameoa.
Itakumbukwa kwamba Upadre
katika Kanisa la Katoliki humtaka anayesomea wito huo asahau kabisa suala la
kuwa na familia, hivyo kwa Domician lilikuwa ni suala gumu mno katika maisha
yake. Alipotoka Nairobi alirudi mkoani Kilimanjaro na kuanza maisha yake katika
eneo moja mkoani humo linalijulikana kwa jina la KIA akiwa na familia moja
wazawa wa Lindi ambao walimlea na kumshawishi asomee masuala ya Utalii katika
chuo kimoja mjini Arusha, hiyo ilikuwa mwaka 2000-2001 alipochukua Masomo ya
Utalii, Ngazi ya Cheti (Tour Guide).
Akiwa mjini Arusha alikuwa
akisoma masomo ya mbali ya Bussiness Administration katika ngazi ya Stashahada yaliyokuwa
yakitolewa na chuo kimoja nchini Uingereza. Mwaka 2001 aliingia mjini Holili na
kuanza masuala ya “Clearing & Forwading”, na baadaye kupata wazo la
kuanzisha Klabu ya Riadha. Ikumbukwe kwamba wazazi wake walifariki akiwa darasa
la tano (5) hiyo ilikuwa mwaka 1984.
No comments:
Post a Comment