Ujumbe wa Holili Youth
Athletics Club (HYAC) umewasili makao makuu ya wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro
ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Klabu hiyo Domician Genandi.
DOMICIAN
GENANDI, MKURUGENZI MTENDAJI HYAC AKISAINI KITABU CHA WAGENI
AFISA
MICHEZO ROMBO GILBERT MANYAGA, MKURUGENZI MTENDAJI HYAC DOMICIAN GENANDI, MKUU
WA WILAYA ROMBO ANAEL PALLANGYO NA OPERATION MANAGER HYAC NELSON MRASHANI
Ujumbe huo uliwasili mapema
asubuhi ya leo ukiwa na malengo ya kukutana na Uongozi wa Wilaya hiyo
kuitambulisha klabu pekee ya riadha nchini ya HYAC.
Akizungumza baada ya kuwasili
katika makao makuu ya wilaya ya Rombo, Domician Genandi alisema HYAC imeasisiwa
katika kijiji cha Holili kilichopo wilayani humo hivyo ni vema watawala wa eneo
hilo wakaijua kwa madhumuni ya kuunga juhudi zinazofanywa na klabu hiyo.
Ujumbe huo ulipokelewa na Afisa
Michezo wa wilaya hiyo Gilbert Manyaga na kasha kupelekwa kwa Afisa Tawala
Emmanuel Buluge.
Mkuu wa Wilaya ya Rombo Anael Pallangyo
alisifu juhudi za HYAC kwani ni ujuasiri kujitambulisha kwa mambo mazuri
yanayofanywa na klabu hiyo kutokana na ukweli kwamba kufanya vizuri kwa HYAC
kumeiinua wilaya hiyo medani ya riadha kwa ujumla.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya Rombo Anthony Tesha alisema kuna ulazima wa halmashauri
yake kuunga mkono juhudi hizo kwani HYAC amekuwa akiisikia katika vyombo
vya habari ikiwa na malengo mazuri ya
kuinua mchezo wa riadha.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa
wilaya ya Rombo, Judatede Mboya alisisitiza umuhimu wa kuwa na mbio maarufu
itakayokuwa ikifanyika katika wilaya yake ikiwa na madhumuni ya kuongeza ajira
na kuinua vipaji hali kadhalika kuitangaza Rombo na Mlima Kilimanjaro.
No comments:
Post a Comment