HYAC

Attack with Style, Defend with Heart

Wednesday, 16 April 2014

HAYATI EDWARD MORINGE SOKOINE NA SOKOINE MIN MARATHON



Biography
 EDWARD MORINGE SOKOINE, ENZI ZAKE AKIWA NCHINI CHINA






 MAZINGIRA YA SASA, MONDULI JUU, KIJIJINI KWA HAYATI EDWARD SOKOINE



 HAYATI EDWARD SOKOINE VITA VYA KAGERA 1978



 HAYATI EDWARD SOKOINE AKIWA KIONGOZI WA KWANZA WA MAPINDUZI FIDEL CASTRO




 DEREVA WA WAZIRI MKUU HAYATI EDWARD MORINGE SOKOINE BAADA YA AJALI

 HAYATI EDWARD MORINGE SOKOINE ALIPOIZURU URUSI

 HAYATI EDWARD MORINGE SOKOINE AKIWA  NA SAMUEL DOE WA LIBERIA

Hayati Edward Moringe Sokoine alizaliwa Agosti 1, 1938 kitongoji cha Kilasho Kijiji cha Emairete Monduli Juu. Kwa wazazi wake, Baba Sokoine Ole Severe na Mama Napelel Sinyati Noomayaki -  Sokoine. Katika Familia yao walikuwa watoto watano. Yeye alikuwa wa tatu kwenye familia.

Kuzaliwa:                           01/08/1938
Kitongoji cha Kilasho, Kijiji cha Emairete, Monduli Juu.
Wazazi:                                Baba Sokoine Ole Severe
                                                Mama Napelel Sinyati Noomoyaki-Sokoine
Elimu ya Msingi:                         1949-1953 Monduli Primary School
                                                1953-1956 Monduli Middle School
Elimu ya Sekondari:      1957-1958 Umbwe Secondary School

Elimu ya Juu:
1962-1963 Mafunzo ya Maofisa Watendaji, Mzumbe
1963-1964 Akiwa Executive Officer alihudhuria mafunzo ya watumishi wa serikali za mitaa nchini Ujerumani
1981-1982 Alijiunga na Chuo Kikuu cha Belgrade, kusomea Uchumi wa Kijamaa alifuzu na kutunukiwa Diploma ya Juu.
1983 Chuo Kiku cha Dar es Salaam (UDSM) kiliyatathmini masomo hayo aliyoyafanya na kuyatambua kuwa ni sawa na shahada ya Bachelor of Arts (BA)
1983-1984 Alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es  Salaam kuchukua masomo ya shahada ya juu ya sayansi ya siasa. Alifariki akiwa amebakiza sura moja kumaliza Thesis yake.

Siasa
Januari 1, 1961 Alijiunga na Chama cha TANU
Februari 5, 1977 Alikuwa mwanachama mwanzilishi wa CCM ilipoanzishwa
1977-1984 Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM
1982 Katibu wa Tume ya Ulinzi na Usalama

Uongozi
1961-1962 Alijiunga na Serikali za Mitaa kama msaidizi wa Katibu  wa Halmashauri ya Shirikisho la Masai (Masai Federal Council), baada ya muda mfupi alipandishwa cheo kuwa Katibu wa Halmashauri ya Shirikisho la Masai.
1963 Baada ya masomo Mzumbe Training Centre, aliteuliwa kuwa Ofisa Mtendaji Daraja la nne.
1965-1970 Mbunge wa Jimbo la Maasai (lililojumuisha majimbo ya sasa ya Ngorongoro, Longido, Monduli, Simanjiro na Kiteto).
1967 Aliteuliwa kuwa Waziri Mdogo (Naibu Waziri) wa Mawasiliano, Uchukuzi na Kazi.
Novemba 1970 Aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais na Waziri Mkuu. 
1970-1980 Mbunge wa Jimbo la Monduli (lililojumuisha majimbo ya sasa Monduli, Longido na Ngorongoro).
Februari 1972 Aliteuliwa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
13/02/1977 -07/11/1980 Aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Novemba 1980 Alijiuzulu wadhifa wa Waziri Mkuu, kwa sababu za kiafya.
1980-1984 Mbunge wa Jimbo la Monduli (Monduli na Longido ya sasa)
Februari 24, 1983 Aliteuliwa kwa mara ya pili kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Nafasi aliyoishika hadi kifo chake Aprili 12, 1984

Marehemu Edward Moringe Sokoine alifariki dunia akiwa Waziri  Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mbunge wa Jimbo la Monduli, Katibu wa Baraza la Ulinzi na Usalama, Mjumbe wa Kamti Kuu na Mjumbe  wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM.

Hayati Edward Moringe Sokoine alifariki akiwa na umri wa miaka 46 na aliacha wajane wawili Mama Napono Sokoine na Mama Nekiteto Sokoine na watoto 11.
Imeandikwa na Jabir Johnson, PRO-HYAC

No comments:

Post a Comment