MONDULI
JUU:
Adelina Audax, mwanariadha chipukizi wa Holili Youth Athletics Club (HYAC) kuchukua
taji la mbio za Sokoine Min Marathon kilometa 2 kwa wasichana mwishoni mwa
wiki.
ADELINA
AUDAX
|
Sokoine Min Marathon ilifanyika
Monduli Juu ikiwa ni Maadhimisho ya miaka 30 tangu kutokea kifo cha aliyekuwa
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Aprili 12, 1984 mkoani Dodoma.
Neema Mathias na Lidiuna
Godfrey walinyakua nafasi za pili na tatu wote wakiwa ni wanariadha chipukizi
kutoka HYAC, nafasi ya nne na tano zilichukuliwa na Susan Patrick (Bala
Secondary School), Sofia Olodi (Okikeso Secondary School).
Kwa upande wa wavulana kilometa
2 Oshun Simon (Nanja Secondary School) alitwaa taji hilo; huku nafasi ya pili
na tatu ikichukuliwa na vijana kutoka Shule ya Sekondari ya Moita ambao ni
Kalei Mereso na Ngoyai Ormeki.
Sabero Naisike wa Shule ya
Sekondari ya Orkeswa alishika nafasi ya nne na nafasi ya tano ilichukuliwa na
Lengarusi Tpasoi wa Shule ya Sekondari Nanja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Holili
Youth Athletics Club, Domician Genandi alisema anafurahi kuona chipukizi
aliowaandaa wanafanya vizuri katika medani ya riadha katika michuano hiyo.
Genandi aliongeza kusema
Sokoine Min Marathon inaweza kuinua vipaji vya riadha kuanzia shule za msingi
hasa ikizingatia kulionekana vipaji vizuri vya mbio hizo, ambavyo vikitafutiwa
mazingira vinaweza kuing’arisha medani ya
riadha nchini.
Hata hivyo alitaka mbio za
Sokoine Min Marathon zitengewe siku yake ili kuleta ladha zaidi hususani kwa
masuala ya kiuchumi watu wa eneo hilo waweze kufanya biashara zao kwa uhuru
hasa ikizingatiwa kwamba “Sokoine Day” hutawaliwa na shughuli nyingi za
kisiasa.
Itakumbukwa kwamba Hayati
Edward Moringe Sokoine alizaliwa Agosti 1, 1938 Kilasho Kijiji cha Emairete
Monduli Juu mkoani Arusha kwa wazazi wake Baba Sokoine Ole Severe na Mama
Napelel Sinyati Noomoyaki.
No comments:
Post a Comment