Wanariadha wawili kutoka Holili
Youth Athletics Club wanatarajiwa kukimbia mbio fupi katika kuadhimisha miaka
50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibari Jijini Dar es Salaam siku ya
Jumamosi.
Wanariadha hao ni Elibariki
Buko na Wambura Lameck ambao watakimbia mbio za mita 800 na 1500
Itakumbukwa kuwa Elibariki Buko
alikimbia Sokoine Min Marathon 2014 kilomita 10 ikiwa ni sehemu yake ya
kujipanga vizuri kuelekea kuadhimisha miaka 50 ya Muungano wa Tanzania, na
kushika nafasi ya 17 kati ya wanariadha 200.
Wambura Lameck ana rekodi ya kufanya
vizuri katika mashindao ya kimataifa hasa ikizingatiwa kwa mara ya kwanza
kushiriki michuano ya kimataifa ilikuwa ni mwezi Machi mwaka huu nchini Uganda
akishika nafasi ya 16 katika kilomita 8 kati ya wanariadha 150 walioshiriki
mbio hiyo.
Wambura Lameck anatarajiwa
mwanzoni mwa mwezi ujao kutua nchini Sweden kwa michuano ya kimataifa akiwa ni
miongoni mwa wanariadha kutoka nchini Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Holili
Youth Athletics Club, Domician Genandi amesema anatarajia kuona vijana wake
wakifanya vizuri katika mbio hizo kwani wana vipaji vinavyoweza kuufanya mchezo
wa riadha kutazamwa kama ilivyokuwa mika ya 1960.
Imetolewa
na:
Jabir
Johnson
Afisa
Habari, Holili Youth Athletics Club
+255-(0)-768
096 793
No comments:
Post a Comment