Unapozungumzia Riadha ni neno
jumla ambalo limekusanya michezo mingi, kwa lugha ya kiingereza wanapozungumzia
riadha huwekwa katika Neno moja “athletics”
.
Asili ya neno hili imetoka kwa
Wayunani ambapo kulitokea maneno maneno mawili ATHLON (θλον) ikiwa na maana ya Zawadi (prize, award) na ATHLOS (θλοс) yenye maana ya
Mashindano (competition).
Athletics imekusanya michezo
kama Kukimbia (Running), Kuruka (Jumping), Kurusha (Throwing) na Kutembea (Walking).
Hata hivyo kuna aina kuu za
Riadha ambazo ni Track and Field, Road Running, Cross Country na Race
Walking.
Hivyo basi kukumbusha tu ni
kwamba mchezo wa Riadha ndio mchezo miongoni mwa michezo inayopendwa na
kushindaniwa hapa ulimwenguni.
Riadha ni mchezo wa kipekee
ambao hushindaniwa na mtu binafsi
ukilinganisha na michezo mingine ukiachia Relay
Races ambazo zimekuwa zikishindaniwa kama timu.
Kwa kifupi ni kwamba mchezo huu
unalipa kwani mafanikio yanapopatikana kwa mtu mmoja pekee hung’arisha jamii
kubwa ya watu anapotoka mchezaji husika.
Imetayarishwa
na CEO Domician R. Genandi, HYAC
tatzo letu wayanzania no kuwa waongo na wanafiki. mfano bajet ya riadha inaweza kuwa 100m, lkn tutaiambia serikali 500m. matokeo ni kuachana nayo kwa kuhofia wingi wafedha na matokeo yatakayopatikana. riadha muwe wakweli daima badala ya usanii.
ReplyDelete