Miaka
ya 1980, nchini Kenya wakati huo Rais wa nchi hiyo alikuwa ni Daniel Arap Moi
ambaye alikuwa akitawala akipokea madaraka kutoka kwa Mtangulizi na Mwasisi wa
Taifa hilo Jomo Kenyatta.
Alichokifanya
Moi aliutazama mchezo wa riadha nchini mwake na kuona kwamba unahitaji
kufanyiwa mabadiliko ya hali ya juu ili kuiwezesha nchi hiyo kufanya vizuri
kimataifa.
Aliyaita
makampuni mawili akayaambia yauwezeshe mchezo huo kupanda kwa kiasi kikubwa,
makampuni hayo mara baada ya kupewa rai hiyo yalianza kazi mara moja na ndio
Kenya unayoiona hii leo ikifanya vizuri katika mchezo huo.
Kumekuwa
na ubishani kwamba siasa haitakiwi katika michezo kwani ikiingia itasababisha
madhara makubwa na hata michezo yenyewe isifanikiwe.
Lakini
leo nasema “Siasa ndio kila Kitu” lakini je inatekelezwaje katika medani ya
michezo.
Tumekuwa
tukipiga kelele kuhusu mchezo wa riadha katika nchi ya Tanzania tangu enzi za
kina Filbert Bayi, Suleiman Nyambui na wengineo waliandika historiakatika
riadha ya Tanzania.
Moi
aliongea tu na makampuni mawili tu na mambo yakenda vizuri, sasa
inashindikanaje kwetu Tanzania ambako hakika tumejaliwa kuwa na hazina ya kila
kitu.
Tulichokosa
katika riadha yetu nimaamuzi ya kiongozi
wetu mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa mwenye hadhi ya
kimataifa Jakaya Mrisho Kikwete.
Sio
lazima mheshimiwa Rais useme na vyombo vya habari tuje ila ni muhimu ukiona
vyema kuita vyombo vya habari, kubwa zaidi ni kuyaita makampuni nchini kuwekeza
katika Riadha.
Mheshimiwa
Rais, binafsi nakupenda sana kutokana na uwezo wako wa kuweza kushawishi katika
mambo mbalimbali, sasa ningekuomba ufanye na hili na kama ujuavyo muda wako wa
kukaa madaraka ndio huo unapunga mkono.
Nimemzungumzia
Moi kwasababu katika riadha alithubutu kufanya licha ya udhaifu wake katika
serikali wakati ule hadi alipotolewa na Mwai Kibaki kupitia NARC, wakenya
wanamkumbuka kwa hilo.
Kwako
Kikwete ni muhimu ukafanya hivyo licha ya kutuletea Kombe la Dunia, UEFA
Champions League kuzuru nchini lakini kumbuka jambo moja kwamba riadha ndio
mchezo pekee ulileta medali nchini Tanzania.
Napolean
Hill katika kitabu chake cha “Think, and Grow Rich” anaandika kwamba ukiweza kufikiria katika mwono sahihi,
utajiri utakuja pasipo mashaka.
Robert
Kiyosaki katika kitabu chake cha “Cashflow Quadrant” anasema kuwekeza katika masuala fulani
husababisha maendeleo katika jamii husika, lakini hiyo inawataka watu wanajua
nini maana ya kuwepo ulimwenguni.
Haina
haja ya maandamano kuja kwako ikulu kukushinikiza Mheshimiwa Rais kuongea na
makampuni maana wewe ndio mpini wa Tanzania hakuna wa kuleta “fyoko fyoko”
ukishasema, Baba Sema Basi!!!! Wanao wazalendo wa Tanzania tujivunie Utaifa
wetu.
Imeandikwa na Johnson Jabir, Columnist
No comments:
Post a Comment