KATIBU WA CHAMA CHA
RIADHA TANZANIA (RT) SULEIMAN NYAMBUI AKISISITIZA JAMBO
|
MOSHI: (JAIZMELALEO) - Mjadala wa wazi kuhusu riadha nchini
Tanzania “RIADHA HARD TALK 2014”
ulioandaliwa na Holili Youth Athletics Club (HYAC) ya mkoani Kilimanjaro
umefanyika jana Februari 9, mwaka huu huku ikibainika wachezaji na makocha
wamekuwa wakiilalamikia serikali na Chama cha Riadha (RT) kutokana na elimu zao
kuwa za kiwango cha chini.
Akizungumza
katika mjadala huo uliofanyika mjini Moshi, Katibu Mkuu wa RT, Suleiman Nyambui
alisema kwa takribani miongo miwili kumeibuka tabia ya watanzania wakiwemo
makocha na wachezaji wa mchezo huo kuilalamikia serikali na RT kutowekeza vya
kutosha katika riadha.
Nyambui
alisema serikali imekuwa ikilalamikiwa kuwa haitaki kuwekeza katika mchezo wa
riadha, wakati huo huo RT nayo ikilalamikiwa kwa kutosimama imara.
“Tuwe
wakweli mbele za Mwenyezi Mungu na atutazame sasa, inakuwaje watanzania,
makocha na wachezaji kulalamika kila kukuchapo kuhusu mchezo wa riadha lakini
kinachoonekana uvivu wa kufikiri na kiwango cha elimu kuwa duni kwa watanzania
ndio kimesababisha lawama kwa serikali na RT” alisema Nyambui.
Hata
hivyo Nyambui aliwataka makocha na wachezaji kuacha kutupa lawama kwa serikali
na RT kutokana na ukweli kwamba wengi wao hawataki kuongeza viwango vyao vya
elimu hali inayosababisha wawe waoga katika kutoa maoni yao.
“
Ukiwa umesoma hautakuwa mwoga katika kutoa maoni yako mahali husika kwa hekima
na busara, kama ni kocha utakuwa ukifundisha kwa weledi tofauti na ilivyo sasa
ambapo makocha wenye sifa za kufundisha mchezo huo wapo wachache hata wengine
kugeuka kuwa madebe matupu yaliapo upepo ukivuma” aliongeza Nyambui.
No comments:
Post a Comment