HYAC

Attack with Style, Defend with Heart

Friday 15 August 2014

FOMU ZA KUJIUNGA NA HOLILI YOUTH ATHLETICS CLUB



 FOMU YA KUJIUNGA
1)     Jina la Mchezaji…………………………………………………..
2)    Umri wa Mchezaji………………………………………………..
3)    Alikozaliwa…………………………………………………………
4)    Uraia………………………………………………………………….
5)    Anakotokea kwa sasa:
Kijiji……………………………………………………………………
Kata……………………………………………………………………
Wilaya…………………………………………………………………
Mkoa…………………………………………………………………..

6)    Anuani……………………………………………………………………………………………………………………..
7)    Namba ya simu………………………………………………………………………………………………………
8)   Jina la Mlezi/Mdhamini…………………………………………………………………………………………
9)    Mawasiliano ya Mlezi/Mdhamini………………………………………………………………………..
10)           Afisa Michezo wa Wilaya/Mkoa…………………………………………………………………….
11) Una matatizo yoyote ya kiafya 
(thibitisha kupitia vyeti vya kidaktari na muhuri wa hospitali      husika)……………………………………………………………………………………………………………............................................................................................
12)            Historia yako ya riadha
    (Je, umewahi kushiriki mashindano yoyote?)
………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

 
MASHARTI YA HOLILI YOUTH ATHLETICS CLUB (HYAC)
Wajibu wa jumla wa mwanariadha
·         Kuheshimu haki, usawa na utu kwa kila mwanariadha, kocha, benchi la ufundi na wote wanaohusika katika klabu hii, usifanye upendeleo.
·         Unapaswa kuwa na maadili, kama mchezaji unapokuwa nje ya uwanja pia ndani ya riadha kwa ujumla.
·         Una wajibu wa kutoa ushirikiano kwa makocha, benchi la ufundi, mameneja wa timu, madaktari wa timu, wawakilishi wa klabu na viongozi wa nchi kwa faida ya mchezaji mwenyewe na klabu.
·         Unapaswa kuwa balozi mzuri unayejali kanuni za mchezo wa riadha, usiende kinyume nazo pia usitumie madawa yaliyokatazwa katika mchezo wa riadha.
·         Unapaswa kutoa taarifa kwa kocha wako, kuhusu maendeleo yako katika mazoezi kama yalivyopangwa kama kuna faida yoyote unayoipata au la.
·         Unapaswa kuwa na vifaa vya mchezo husika, tangu siku ya kwanza unapojiunga (kama ilivyoanishwa katika fomu hii), na ukisha kubaliwa unatakiwa kufuata ratiba ya klabu kwa wakati.
·         Mara zote toa shukrani kwa makocha na maafisa wengine wa klabu pindi unapokuwa katika mazoezi au michuano.
·         Epuka kutumia kauli mbaya, ikiwemo kuapa au kuwa na tabia hatarishi kwako na kwa wanariadha wengine, epukana na fujo, ugomvi na kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi na mwanariadha wa klabu.
·         Unapotaka kuhamia klabu nyingine ya riadha, taarifa ni lazima zifike katika ngazi ya utawala kwa maandishi ili kufikia makubaliano ya pande zote mbili.
·         Utakaporuhusiwa kujiunga na klabu utapewa sheria za jumla za kambi na kwenye michuano mbalimbali.

Mahitaji ya awali ya mwanariadha atakapokubaliwa maombi ya kujiunga na klabu:
·         Truck suit jozi 1 au 2
·         Bukta jozi 2 na zaidi
·         Viatu vya mazoezi jozi 2
·         Viatu vya mashindano jozi 2
·         Kiasi cha pesa zako binafsi kwa ajili ya kujikimu katika siku za mwanzo
·         Picha passport size 2 kwa ajili ya kumbukumbu za ofisi
·         Shuka na blanketi

  
NB: Kama unakubaliana masharti haya thibitisha kwa kuandika neno NDIO katika nafasi iliyopo………………………..

Saini ya Mchezaji……………………………….
Tarehe……………………………………………..

Saini ya Mzazi/Mlezi………………………….
Tarehe …………………………………………….

Saini ya Mdhamini……………………………..
Tarehe …………………………………………….

Saini ya Afisa michezo Wilaya au Mkoa (muhuri na saini kuthibitisha)……………………….…………………………
Tarehe ……………………………………………..

KARIBU SANA

©
Holili Youth Athletics Club (HYAC)

No comments:

Post a Comment