HYAC

Attack with Style, Defend with Heart

Tuesday 8 April 2014

UJUMBE HYAC WATINGA OFISI ZA WILAYA YA ROMBO



Ujumbe wa Holili Youth Athletics Club (HYAC) umewasili makao makuu ya wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Klabu hiyo Domician Genandi.

 DOMICIAN GENANDI, MKURUGENZI MTENDAJI HYAC AKISAINI KITABU CHA WAGENI




 AFISA MICHEZO ROMBO GILBERT MANYAGA, MKURUGENZI MTENDAJI HYAC DOMICIAN GENANDI, MKUU WA WILAYA ROMBO ANAEL PALLANGYO NA OPERATION MANAGER HYAC NELSON MRASHANI





Ujumbe huo uliwasili mapema asubuhi ya leo ukiwa na malengo ya kukutana na Uongozi wa Wilaya hiyo kuitambulisha klabu pekee ya riadha nchini ya HYAC.

Akizungumza baada ya kuwasili katika makao makuu ya wilaya ya Rombo, Domician Genandi alisema HYAC imeasisiwa katika kijiji cha Holili kilichopo wilayani humo hivyo ni vema watawala wa eneo hilo wakaijua kwa madhumuni ya kuunga juhudi zinazofanywa na klabu hiyo.

Ujumbe huo ulipokelewa na Afisa Michezo wa wilaya hiyo Gilbert Manyaga na kasha kupelekwa kwa Afisa Tawala Emmanuel Buluge.

Mkuu wa Wilaya ya Rombo Anael Pallangyo alisifu juhudi za HYAC kwani ni ujuasiri kujitambulisha kwa mambo mazuri yanayofanywa na klabu hiyo kutokana na ukweli kwamba kufanya vizuri kwa HYAC kumeiinua wilaya hiyo medani ya riadha kwa ujumla.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Rombo Anthony Tesha alisema kuna ulazima wa halmashauri yake kuunga mkono juhudi hizo kwani HYAC amekuwa akiisikia katika vyombo vya  habari ikiwa na malengo mazuri ya kuinua mchezo wa riadha.

Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya ya Rombo, Judatede Mboya alisisitiza umuhimu wa kuwa na mbio maarufu itakayokuwa ikifanyika katika wilaya yake ikiwa na madhumuni ya kuongeza ajira na kuinua vipaji hali kadhalika kuitangaza Rombo na Mlima Kilimanjaro.

No comments:

Post a Comment