HYAC

Attack with Style, Defend with Heart

Saturday 30 November 2013

WATANZANIA WAWILI KUKIMBIA PUNE INTERNATIONAL MARATHON DESEMBA MOSI



Michuano ya Pune (Poona) International Marathon inatarajiwa kufanyika kesho Jumapili (Desemba Mosi 2013) nchini India, huku Tanzania ikiwakilishwa na wanariadha wawili tu kutoka katika Klabu ya Holili Youth Athletics.
 
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari mapema leo mchana imesema wanariadha hao ambao walianza safari yao Novemba 27, mwaka huu ni Oswald Revelian Kahuruzi ambaye anashiriki mbio hizo kwa mara ya 3 na Pascal Mombo Sarwat ambaye ni mara yake ya kwanza kushiriki mbio hizo.

Rais wa Holili Youth Athletics Domician Rwezaura alisema Oswald Kahuruzi atakimbia mbio hizo katika umbali wa Kilometa 42 wakati Sarwat atakimbia Half Marathon ambayo ni Kilometa 21.

Blogu hii ilifanya mahojiano nao majira ya saa 3:35 asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki kwa saa za India ilikuwa ni saa 6:35 mchana kuhusu mustakabali wao katika mbio hizo hasa ikizingatiwa wao ni watanzani a pekee wanaoipeperusha bendera.

Kwa pamoja wanaraidha hao walisema changamoto ni kubwa kutokana na ukweli kwamba hali ya hewa kwa sasa katika mji huo ni joto hivyo watajitahidi kuipeperusha bendera.

Hata hivyo walibainisha kuwa nchi mahiri duniani kwa kutoa wanariadha ambazo ni Ethiopia na Kenya zimeleta wanariadha wengi ikilinganisha na Tanzania.

Ethiopia imewaleta wanariadha 100 na Kenya ikiwa na wanariadha 48.
Itakumbukwa kwamba Pune ni mji ulio karibu kabisa na Jiji Mahiri nchini India la Mumbai.

Friday 29 November 2013

DICKSON MARWA KUONGOZA UHURU MARATHON



http://www.apb.se/preview/070827_2909.jpgMWANARIADHA mahiri, Dickson Marwa, anatarajiwa kuwaongoza wanariadha wengine 10 kuipeperusha bendera ya Klabu ya Riadha ya Holili, ‘Holili Youth Athletic Club (HYAC)’, kwenye mbio za kwanza za Uhuru Marathon zitakazotimua vumbi Desemba 8 jijini Dar es Salaam.

Dickson ambaye kwa sasa ni moto wa kuotea mbali katika mbio za kilomita 21 (Nusu Marathon), atawaongoza wenzake Nelson Priva, Alfonce Felix, Saidi Makula, Lucian Reginald, Catherine Lange, Fadhila Salum, Consolata Samwel, Selina Amos na Augustino Sulle katika kilomita 21 pamoja na Dotto Ikangaa atakayeshiriki kilomita 5.

Mkurugenzi mtendaji wa klabu hiyo, Domician Rwezaura, katika mahojiano maalumu ofisini kwake alisema kwamba Marwa na wenzake wataondoka Desemba 7 wakiongozana na viongozi wanne akiwemo kocha wao, Adram Mikumi, Meneja Nelson Mrashani, na Katibu Innocent pamoja na mwenyewe.

Rwezaura alisema, mazoezi yanaendelea katika kambi ya mazoezi yaliyoko Tarakea.

Wakati huohuo, fomu za usajili wa mbio za Uhuru Marathon zimeanza kutolewa siku ya Jumapili  katika ofisi za klabu ya Holili zilizoko katika jengo la Plaza, mkabala na stendi ndogo ya mabasi ya mjini Moshi.

EDNA KIPLAGAT KUSHIRIKI UHURU MARATHON DESEMBA 8



http://dt9guucc6nuua.cloudfront.net/media/LargeP/6e9475ea-87f8-4530-8848-e169b907562a.jpg?v=-1170362114
UHURU MARATHON inatarajiwa kufanyika Desemba 8, 2013 Jijini Dar es Salaam. Wanariadha mbalimbali nchini na nje ya nchi wanatarajiwa kushiriki akiwemo Edna Kiplagat ambaye ni Bingwa wa Dunia wa Michuano ya IAAF ya mwaka 2011 na 2013.
Edna Kiplagat ataungana na wakimbiaji wengine 16 kutoka nchini Kenya.

Holili Youth Athletics Club ya Mkoani Kilimanjaro ni klabu pekee nchini Tanzania yenye mzigo na wakimbiaji wa riadha hapa nchini nayo itapeleka wanaridha katika michuano hiyo.

Itakumbukwa kwamba Edna Kiplagat alishiriki mbio za Los Angeles na New York City mwaka 2010.

CHANZO: JAIZMELALEO

HOLILI YOUTH ATHLETICS CLUB (HYAC)



HOLILI YOUTH ATHLETICS CLUB
(HYAC)
http://1.bp.blogspot.com/-9InwZ5RVHW0/Ua8g-RS7jbI/AAAAAAAAmJU/6UPwPogsj9E/s1600/holili+2.JPG
P.O BOX 273 HOLILI-KILIMANJARO
TEL: +255-(0)- 784 474 130/ 0759 115 932; 0754 806 283/ 0782 573 880; 0768 096 793
“Sports brings people together, Come and Join us”
INTRODUCTION
Holili Youth Athletics Club is the Club which started its athletics activities in 2010 and it was officially registered on 25th October 2011 with registration N.S.C No. 9833.
LOCATION
Holili Youth Athletics Club (HYAC) is located at Holili Town, in Rombo District 36 km from Moshi Town at the border of Tanzania and Taveta-Kenya.
VISION
Holili Youth Athletics Club (HYAC) is one of the institution deals in developing athlete talents among youth men and women the rest of the country.
MISSION
  1.  To enable and unfold youth potential talents in athletics through training and exposing him or her in different competitions to enhance skills and experience.
  2.  To stimulate and promote Athletics activities in Tanzania by enabling youth to participate in various competitions so as to strengthen their destiny.
OBJECTIVES
1.        Financial support highly needed, simply because The Club recruits  and trains the athletes, (solicit enough money for running the centre-competitions, meals and transport).
2.      Orphanage, Holili Youth Athletics Club targets this group by aspiring their talents and be able to perform hence become champions.
3.       To supply athletes with sports items, provide food, transport and accommodation for training and competition.
Holili Youth Athletics Club is ready to fulfill your dreams and vision, come and join us.
http://3.bp.blogspot.com/-pN0s_w_5ZNw/UV2isJZ4fyI/AAAAAAAAj-k/FyzNh6BfiGw/s640/DSC01539.JPG
PHOTO: JOHNSON JABIR AND PRESIDENT DOMICIAN "GENANDI" RWEZAURA 

Written by: JOHNSON JABIR, November 29, 2013