HYAC

Attack with Style, Defend with Heart

Friday 30 January 2015

HOLILI YOUTH YASHIRIKI UZINDUZI KILI MARATHON 2015, MOSHI



 Director de Holili Juventud Atletismo Club (HYAC) Domician Genandi, llega a Palacio de Kibo para inaugration Maratón de Kili 2015. 


Klabu ya Riadha ya Holili Youth (HYAC) imeshiriki katika shughuli za uzinduzi wa mbio za Kili Marathon mwaka huu katika viunga vya Kibo Palace Home mjini Moshi jana ikiongozwa na mkurugenzi wa klabu hiyo Domician Genandi.

Ujumbe wa watu 8 kutoka klabu hapo uliwasili katika viunga vya Kibo Palace Home ambapo Mgeni rasmi alikuwa Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro Severin Kahitwa akimwakilisha mkuu wa mkoa.

Holi Youth (HYAC) ilikaribishwa na baada ya hafla hiyo kumalizika waliwekea mkanda uliokuwa ukielezea ushiriki wa klabu hii katika kuinua vipaji  vya riadha hapa nchini na ushiriki wao katika Kili Marathon mwaka uliopita.

Wadhamini wa Mbio hizo mwaka huu ni Kilimanjaro Premier Lager ambapo wanadhamini kilometa 42, Tigo kilometa 21 na GAPCO wanamichezo wasiojiweza, wenye mahitaji maalum.
Kibo Palace Home inamilikiwa na Laswai miongoni mwa wafanya biashara maarufu mkoani Kilimanjaro.














Monday 26 January 2015

UNGA MKONO JUHUDI ZA KUINUA RIADHA NCHINI



 Genandi Rwezaura, Caren Rwezaura na Geoffrey wakiwa Holili, Kilimanjaro


Sasa ni umri wa kwenda shule, watoto hawa wanahitaji matunzo mazuri ili matarajio yao yawe kamili hapo baadaye; tunawategemea sana katika kuinua riadha siku zijazo. 

Unga mkono juhudi za kuinua riadha nchini Tanzania kwa kuwa miongoni mwa watu wanaohamasisha jamii, kuwekeza katika mashule ili kupata vipaji vilivyokomaa kwa ajili ya kuung’arisha mchezo wa riadha kimataifa.

Klabu ya Riadha ya Holili Youth (HYAC) ni miongoni mwa wadau muhimu wanaoinua riadha nchini Tanzania.

Friday 23 January 2015

UMOJA, UPENDO, FURAHA, AMANI NGUZO MUHIMU HOLILI YOUTH



 Ludwina Godfrey, Michael Nkwabi, Pascalina Slyvester, Lameck Misiwa,  Deogratius Lazaro


Umoja, Upendo, Furaha, Amani ni miongoni mwa mambo ambayo huweza kufanikisha mambo mengi katika kundi la watu au jamii husika.

Wanariadha wa klabu ya riadha ya Holili Youth (HYAC) iliyopo katika kijiji cha Holili wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro wamejaliwa kuwa na mambo hayo.

Wakati wote hufurahi, kila mmoja akiwa na amani na mwenzake hali ambayo imekuwa ikifanikisha sana utendaji wa klabu hiyo.

Ikumbukwe kwamba HYAC imejielekeza zaidi katika kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji vya vijana wanaopenda mchezo wa riadha.

Kwa miongo kadhaa sasa medani ya riadha nchini imepoteza mwelekeo hali ambayo imekuwa ikishusha mwamko wa vijana.

Hii imetokana na ukweli kwamba serikali imeshindwa kuelekeza nguvu zake katika shule za msingi na sekondari ambako kuna vijana chipukizi wanaoweza kuiletea sifa nchi ya Tanzania katika medani hii adhimu.

Hata hivyo licha ya kusuasua huko bado jitihada za mmoja mmoja zinaendelea ikiwemo vilabu mbalimbali nchini kuwa na ari ya kuinua mchezo husika.

Holili Youth Athletics Club (HYAC) ni miongoni mwa wadau muhimu wa mchezo wa riadha licha ya ukosefu wa wafadhili katika maeneo mbalimbali.

Imejitahidi kuweka kambi ambako nyota wa mchezo huo huendelea kufanya mazoezi ya pamoja.
 Lameck Misiwa, Michael Nkwabi,Furaha Sabaya, Deogratius Lazaro na Ludwina Godfrey


 Deogratius Lazaro


 Furaha Sabaya na Michael Nkwabi


 Furaha Sabaya


 Rehema, HYAC matron in the camp

 Lameck Misiwa

 Ludwina Godfrey

 Michael Nkwabi

 Pascalina Slyvester na Adelina Audax

 Pascalina Slyvester, Adelina Audax na Neema Mathias

Thursday 15 January 2015

PASCALINA SYVESTER KUJIUNGA NA HOLILI



PASCALINA SLYVESTER (KUSHOTO) AKIWA NA MWALIMU JAMBAU AMBAYE ALIKUWA AKIMNOA AKIWA SINGIDA



Mwanariadha Chipukizi Pascalina Slyvester (17) kutoka Singida anatarajiwa kujiunga na wanariadha wengine wa Holili Youth Athletics Club (HYAC) katika mazoezi ya kujiandaa na michuano mbalimbali mwaka huu.

Nyota huyo chipukizi wa mbio fupi na za kati alionwa na klabu hiyo katika mbio za Rotary Marathon 2014 Jijini Mwanza alipotimua mita 1500.

Klabu ya riadha ya Holili Youth inaendelea na kampeni zake za kutafuta vipaji vya riadha nchini kwa maendeleo ya mchezo wenyewe na taifa kwa ujumla.

Pascalina atajiunga katika kambi ya mazoezi ya Holili iliyopo wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro.
 PASCALINA SLYVESTER AKIKABIDHIWA TUZO BAADA YA KUMALIZIA WA TATU KATIKA KARATU SPORTS FESTIVAL 2014 MKOANI ARUSHA