HYAC

Attack with Style, Defend with Heart

Thursday 27 February 2014

RT YAIPONGEZA HYAC KWA "RIADHA HARD TALK 2014"



HOLILI YOUTH ATHLETICS CLUB IMEPEWA PONGEZI NA CHAMA CHA RIADHA NCHINI TANZANIA KWA KUENDESHA MDAHALO WA WAZI FEBRUARI 9, 2014 ULIPEWA JINA LA " RIADHA HARD TALK 2014"
Barua ya RT Kumb. Na. RT/Vol.4/13/SNM/53
Hata hivyo katika barua hiyo iliyotolewa na Katibu Mkuu wa RT Suleiman Nyambui ilitoa wito wa kufanyika kikanda nchi nzima ili kukuza uelewa wa mchezo wa riadha

Saturday 15 February 2014

RIADHA NI NINI?



Unapozungumzia Riadha ni neno jumla ambalo limekusanya michezo mingi, kwa lugha ya kiingereza wanapozungumzia riadha huwekwa katika Neno moja “athletics” .

DOMICIAN R. GENANDI
Asili ya neno hili imetoka kwa Wayunani ambapo kulitokea maneno maneno mawili ATHLON (θλον) ikiwa na maana ya Zawadi (prize, award) na ATHLOS (θλοс) yenye maana ya Mashindano (competition).

Athletics imekusanya michezo kama Kukimbia (Running), Kuruka (Jumping), Kurusha (Throwing) na Kutembea (Walking).

Hata hivyo kuna aina kuu za Riadha ambazo ni Track and Field, Road Running, Cross Country na Race Walking.

Hivyo basi kukumbusha tu ni kwamba mchezo wa Riadha ndio mchezo miongoni mwa michezo inayopendwa na kushindaniwa  hapa ulimwenguni.

Riadha ni mchezo wa kipekee ambao hushindaniwa na mtu  binafsi ukilinganisha na michezo mingine ukiachia Relay Races ambazo zimekuwa zikishindaniwa kama timu.

Kwa kifupi ni kwamba mchezo huu unalipa kwani mafanikio yanapopatikana kwa mtu mmoja pekee hung’arisha jamii kubwa ya watu anapotoka mchezaji husika.

Imetayarishwa na CEO Domician R. Genandi, HYAC

Tuesday 11 February 2014

RT YAIUMBUA SERIKALI YA JK



Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha nchini Tanzania (RT) Suleiman Nyambui ameitolea uvivu serikali na kuitaka iache kuwadanganya watanzania kuhusu mchezo wa riadha ambao umekuwa ukizorota kwa kipindi kirefu sasa.


Akizungumza katika mjadala wa wazi “Riadha Hard Talk 2014” ulioandaliwa na Holili Youth Athletics Club na kufanyika mjini Moshi Februari 9 mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano wa Moshi Club.

Nyambui alisema kwa muda sasa lawama zimekuwa zikiwaangukia chama cha riadha nchini kwamba hawawajibiki hata chembe katika kuinua mchezo huo ambao umeipatia sifa Tanzania miaka ya 1960 hadi 1980.

Katibu huyo aliongeza kusema kuwa miaka ya nyuma serikali ilikuwa bega kwa bega na wanariadha, hali ambayo iliwahamasisha kwa kiasi kikubwa kuinua vipaji vya chipukizi waliokuwa wakisoma shuleni na vyuoni.

“Hali imekuwa tofauti sasa ukilinganisha na miaka ya nyuma wakati tukisoma kwani mwanariadha aliheshimiwa na watu wote hususani viongozi wa serikali tofauti ilivyo sasa”. Alisema Nyambui

Pia Nyambui alisema serikali imeshindwa kusimamia tasnia ya riadha na imebakia kutoa lawama kwa chama cha riadha nchini, kwani mpaka sasa imeanzisha kamati za michezo katika wilaya na mkoa kwa ajili ya kusaidia michezo kwa karibu zaidi lakini hali imekuwa mbaya kutokana na kamati hizo kuwajibika kwa mchezo wa soka pekee huku mingine ikisahaulika.

Aidha Nyambui aliongeza kusema hadi sasa wamejitahidi kupeleka mapendekezo kadhaa baina yao na serikali ili waweze kukaa chini na kufikia suluhisho la namna ya kuinua riadha lakini serikali haijajibu hali inayoonyesha kutotilia maanani. 

Kwa upande wake Kocha wa Kwanza wa riadha hapa nchini Tanzania kutambuliwa na Shirikisho la Riadha Duniani Samwel Tupa alikazia katika mjadala huo kuwa serikali imejisahau sana katika mchezo wa riadha kutokana na ukweli kwamba hata kuwaruhusu  wanariadha wafanye mazoezi katika uwanja wa Taifa limekuwa ni suala lisilokubalika.

Tupa aliongeza kusema uwanja wa taifa wenye vifaa muhimu katika mchezo wa riadha hauna msaada katika kuwainua wanariadha wa Tanzania kufanya vizuri kimataifa.

Kocha huyo alisema  hivi sasa uwanjani hapo kuna baadhi ya alama za riadha zimeanza kufutika kutokana na kutotumika na nyingine hata kufunikwa na nyasi na udongo huku watu wakifurahia rangi ya uwanjani hapo.

“Riadha Hard Talk 2014” iliandaliwa ikiwa na madhumuni ya kukusanya maoni ya nini kifanyike kuinua mchezo wa riadha ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 60 tangu mchezo wa riadha utambulike rasmi nchini Tanzania; ambapo washiriki 60 walihudhuria kati ya 100 walioalikwa.

Monday 10 February 2014

MKE WA WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI AHUDHURIA RIADHA HARD TALK 2014



Riadha Hard Talk 2014 imefanyika huku ikiwa na kumbukumbu ya washiriki kutoa michango yenye kujenga riadha nchini Tanzania.

MAGGIE MLENGEYA
Miongoni mwao ni mke wa Waziri Maggie Mlengeya Kamani aliyekuwepo katika mjadala huo muhimu.



 SAMWEL TUPA, KOCHA WA KWANZA RIADHA NCHINI TANZANIA AKICHANGIA MJADALA HUO

BI. MAGGIE MLENGEYA AKIHOJIWA NA MWANDISHI HABARI BAHATI NYAKIRARIA



BI. MAGGIE MLENGEYA KATIKA VIWANJA VYA MOSHI CLUB

BI MAGGIE MLENGEYA NI MWANDAAJI WA SERENGETI MARATHON 2014 KUHUSU HILO TUTAKULETEA MAKALA IJAYO KUHUSU SERENGETI MARATHON 2014 NA NJIA ZAKE.