HYAC

Attack with Style, Defend with Heart

Thursday 1 May 2014

KONA YA PRO MEI 2014 NA JABIR JOHNSON





Toleo la Mei 2014
Yaliyomo
  1. UTANGULIZI
  2. HOLILI YOUTH ATHLETICS CLUB
  3. UNAWAKUMBUKA?
  4. AFYA NA RIADHA
  5. SURPRISE RIO!
  6. B’E
  7. TO THE BEST
  8. BIOGRAPHY CHAMBER



Kona ya PRO-ni kijarida kidogo cha kwenye mtandao ambacho hutolewa kila ,mwezi na Holili Youth Athletics Club(HYAC). Kimekusanya masuala kadhaa yanayohusu mchezo wa riadha, fuatana nasi hadi mwisho kwa yale tuliyokuandalia kwa mwezi Mei mwaka huu.

Itakumbukwa kwamba riadha ni mchezo unaopendwa na watu wengi ulimwenguni kwani ndio mchezo mama wa michezo mbalimbali ulimwengu. Umekuwa ukihusisha mwili wa binadamu kwa kiasi kikubwa. Pia mchezo huu umekuwa  ukihusisha mtu mmoja mmoja katika ushindani wake ukiachia relay races.

Riadha (Athletics) michezo mbalimbali kama kukimbia (running), kuruka (jumping), kurusha (throwing) na kutembea (walking). Hata hivyo kuna aina tatu za riadha ambazo ni Track and Field, Road Running, Cross country na Race Walking.
 
Domician Genandi
Mkurugenzi Mtendaji
Holili Youth Athletics Club (HYAC).



Domician Rwezaura Genandi ni miongoni mwa mamia ya waanzilishi na wamiliki wa klabu za riadha hapa ulimwenguni wenye shauku ya kuinua mchezo huo ujulikane zaidi, kila pembe ya dunia.Mwanzilishi huyu ndiye pekee mwenye klabu yenye malengo ya kuwainua wanariadha nchini Tanzania hususani vijana wanaochipukia katika mchezo huo.



HYAC inapatikana katika Kijiji cha Holili kilichopo mpakani mwa Tanzania na Kenya katika wilaya ya Rombo ikiwa ni kilometa 36 kutoka Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro. Itakumbukwa kwamba Holili Youth Athletics Club (HYAC) ilianza kujihusisha na masuala ya riadha mwaka 2010 na kusajiliwa rasmi Oktoba 25, 2011. Mwaka 2011 ilijipatia usajili wake kutoka Baraza la Michezo nchini Tanzania (BMT) Na. 9833.


Holili ipo katika miteremko ya Mlima mahiri ulimwenguni wa Kilimanjaro na kambi ya mafunzo kwa wachezaji wake ipo katika Mjini wa Tarakea mpakani mwa Tanzania na Kenya.


Holili Youth Athletics Club (HYAC) inajitahidi kufanya yafuatayo, ikiwa na malengo ya kuuinua vipaji vya wanariadha nchini na mchezo wenyewe kwa ujumla.

Wanariadha wa HYAC, wakijiandaa kukimbia mita 5,000, Kili Marathon 2014 iliyofanyika mjini Moshi.
          Falsafa yetu ni kufanya kazi kwa bidii na kujitoa, Falsafa hiyo inaongozwa na kauli mbiu ya “ Michezo huwaweka watu pamoja, Njoo Ujiunge nasi”(Sports brings people together come and join us).

         Holili Youth Athletics Club inajitoa kwa muda, hali na mali kwa ajili ya kuifanya klabu isonge mbele kwa matokeo mazuri. Hivyo inatarajia mwanariadha ataongeza bidii katika mazoezi ili kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali.

         HYAC ina wafanyakazi ambao sharti wawe waaminifu kwelikweli, ambapo wanatarajia kuona wanariadha wanapofanya vizuri ndio furaha kwao kwani malengo ya kuinuamchezo wa riadha yanafikiwa.

         Hata hivyo klabu hii, pekee ya riadha nchini Tanzania yenye ari na hamasa ya kuinua mchezo wa riadha inaendelea na juhudi za kutafuta ushauri kutoka kwa wanariadha waliowahi kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa kwenye maeneo ambao hawana ufahamu nayo kwa malengo kwamba mwanariadha wa HYAC aweze kupata nafasi ya kusonga mbele.
 


Leo, katika kipengele hiki ninakuletea Wanariadha watano waliovunja rekodi kabla ya mwaka 2005 katika mbio za kilometa 42 (Full Marathon).

NA.
JINA
NCHI
MUDA
MWAKA
MBIO
1
Paul Tergat
KENYA
2:04.55
2003
BERLIN
2
Khalid Khanouchi
MOROCCO
2:05.38
2002
LONDON
3
Khalid Khanouchi
MOROCCO
2:05.42
1999
CHICAGO
4
Ronaldo da Costa
BRAZIL
2:06.05
1998
BERLIN
5
Belayneh Dinsamo
ETHIOPIA
2:06.50
1988
ROTTERDAM
  
MWILI WA BINADAMU
Mwili wa binadamu ni mashine inayoishi na ili kuufahamu vizuri ni muhimu kuusoma jinsi ulivyoundwa, kwa kufanya hivyo itasaidia kukuza mchezo wenyewe.

Makocha wengi wamekuwa wakishindwa kuwafundisha wachezaji wao vipaji, kutokana na uelewa finyu wa namna mwili wa binadamu ulivyo.

Wakati mwingine mchezaji anaweza kutojisikia vizuri kutokana na masuala mbalimbali msichana ama mvulana huku mwalimu akimtaka kuendelea kukimbia wakati viungo vya mwili vimegoma.

Wakimbiaji (athletes) wanaweza kuwa na maumbo na maumbile tofauti, rangi za ngozi zao zikawa tofauti lakini suala la mwili kufanya kazi hufanyika bila kujali hayo kwani wao ni watu walioumbwa kwa mifupa na mishipa.

Huhitaji mpaka uwe daktari kuujua mwili wa binadamu kwa ajili ya mchezo wa riadha, hivyo unaweza kuelewa kupitia “Kona ya PRO” namna gani mwili wa binadamu anavyoweza kufanya kazi.

Mwili wa binadamu umeundwa na mambao yafuatayo:
  • Seli
  • Mifupa
  • Mishipa
  • Neva za Mawasiliano
SELI (Cells)

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjUk0OiUWgOfMl4QppibFI2PAQXD7ycNmGnoun6hjG38V9rnHQQ1ma6uV6IV4rTcA4xkYNCrLzTHBQIrspY4LxmQMIl-mhzMJfQXcsvzuJzpQa4_ni_pZAT43ZFxoPBqO738ngWk2tDrps/s1600/10.jpgViumbe hai vyote vinandwa na seli moja au zaidi. Mwili wa binadamu unaundwa na mamilioni ya seli ndogondogo zinazoishi.

Seli ndizo zinaunda ngozi yetu, mifupa yetu, mishipa, ubongo na vingine vingi katika miili yetu.

Hivyo kila tunachokifanya kinahusisha mamilioni ya seli ndogondogo zinazoishi zenye maumbo na ujazo tofauti ambapo hufanya kazi pamoja kufikia malengo.

Kila aina seli hufanya kazi mbalimbali, ambapo huchukua ujumbe kutoka sehemu moja kwenda nyingine, huchukua kemikali ambazo hubeba hewa ya oksjeni, seli hizo hufanya mwili usimame pia husababisha mwili utembee.

Kila seli hufanya kazi yake, lakini kwa ujumla wake huishi, hukua na hatimaye kufa na seli nyingine huchukua nafasi na kuendelea na jukumu la kuufanya mwili ufanye kazi yake. 

SKELETON
Binadamu, kama walivyo wanyama wakubwa, wana skeleton katika miili yao. Skeleton ni mfumo wa mifupa na vitu vingine vinavyoupa kuutwa mfupa.
Skeleton hufanya kazi tatu ambazo ni
  • Support
Skeleton inafanya kazi kama ambavyo wajenzi huweka msingi ili nyumba isimame. Bila skeleton, mwili wa binadamu usingekuwa na umbo lolote la kueleweka.
  • Protection
Skeleton  inaweka ulinzi wa viungo ambavyo ni laini vinavyoweza kuathirika kwa haraka, kwa mfano moyo ubongo unalindwa na fuvu ambalo ni mkusanyiko wa mifupa.
  • Movement
Skeleton husababisha mwendo baada ya misuli kuunganika na mfupa. Hiyo misuli iliyounganika kwenye mfupa ndio inafanya jointi zifanye kazi. Katika hilo skeleton huweka balance (uwiano sawa) ndipo mwili unaweza kutembea.
Katika masuala ya riadha ni muhimu sana  kuelewa namna ambavyo mwili wa binadamu unaweza kufanya kazi, ili kuleta matokeo chanya kwa mchezaji husika.
Itaendelea toleo lijalo…

Kwa mara ya kwanza, “SURPRISE RIO!” ni kipengele kitakachokuwa kikikuletea matukio ya kushangaza, kuchekesha, kuhuzunisha na wakati mwingine kukupanua ufahamu.
Leo, nitawaangazia wafuatao:

Mwanadada huyo katika mbio za Sokoine Min Marathon Kilometa 2 ambaye hakufahamika jina mara moja.

Huyo ni miongoni mwa waliokimbia kilometa mbili lakini kabla ya kuanza Kona ya Pro iliyasikia maneno ya watani wa mwanadada huyo kuwa , ingekuwa vema aandike kwanza wosia.

Maneno hayo yalikuwa na maana gani? Kumbe walijua wazi kuwa angechoka sana, ndivyo ilivyokuwa, alipokuwa akimaliza mbio hizo Maafisa walimpokea akiwa hoi bin taabani na kumhudumia.

Pili, wanariadha vipaji waliokosa matunzo, Kona ya Pro ilishuhudia jinsi ambavyo wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari wa Kijiji alichozaliwa Hayati Edward Moringe Sokoine wakichuana katika kilometa 2, wasichana kwa wavulana ilikuwa patashika nguo kuchanika.



B’E ni kifupisho cha maneno yafuatayo, “BIG EVENT” . Leo katika kipengele hiki tunakuletea tukio la kimichezo lililokuwa na mvuto kwa mwezi Aprili mwaka huu.

Sokoine Min Marathon 2014

Sokoine Min Marathon 2014 ilifanyika kwa mara ya pili mfululizo kwa ajili ya kuadhimisha miaka 30 ya kifo cha Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine.

Hayati Sokoine alifariki kwa ajali Aprili 12, 1984 mkoani Dodoma. Aprili 12, 2014 ilikuwa ni miaka 30 tangu kutoweka duniani kwa kiongozi huyo ambaye anatajwa kuwa mwadilifu na mzalendo.

Maadhimisho hayo yaliwaleta karibu viongozi mbalimbali wa kisiasa ambao walimiminika akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Jakaya Kikwete, Rais wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Benjamin Mkapa na Waziri Mkuu Aliyejiuzulu wadhifa huo Mheshimiwa Edward Lowassa.

Maalim Seif Sharrif Hamad Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar alihudhuria maadhimisho hayo yaliyopambwa na gwaride kutoka majeshi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Michezo mbalimbali ya Riadha ilifanyika ikiwemo kukimbia mingine ni Kurusha Mkuki na kuruka. 

Holili Youth Athletics Club (HYAC) ilichomoza kwa kishindo katika Sokoine Min Marathon kwa kilometa 2 na kilometa 10.

Adelina Audax, Neema Mathias na Lidiuna Godfrey walichukua nafasi tatu za juu baada ya kuwashinda wanariadha wa kike waliokimbia kilometa 2.

Alphonce Felix alichomoza nafasi ya pili kilometa 10 akiiwakilisha Holili Youth Athletics Club (HYAC) akikimbia kwa muda wa dakika 34:45.39 akiachwa na Fabian Joseph kwa sekunde 16 (34:28.04).

Nafasi ya tatu ilishikwa na Bingwa wa Sokoine Min Marathon 2013, Dickson Marwa (HYAC) akikimbia kwa dakika 34:57.47

Kwa wanawake kilometa 10 mwanadada Jackline Sakilu, Bingwa Kili Marathon 2014 kilometa 21, alitwaa taji hilo akiliwakilisha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) akikimbia kwa dakika 40:01.26 akifuatiwa na Nathalia Elisante kutoka mkoani Arusha akitumia muda wa dakika 40:51.27 na nafasi ya tatu ilinyakuliwa na Failuna Abdi kutoka Winning Spirit Arusha akifukuza upepo kwa dakika 41:13.54

Kwa upande wa wavulana kilometa 2 Oshun Simon (Nanja Secondary School) alitwaa taji hilo; huku nafasi ya pili na tatu ikichukuliwa na vijana kutoka Shule ya Sekondari ya Moita ambao ni Kalei Mereso na Ngoyai Ormeki.

Sabero Naisike wa Shule ya Sekondari ya Orkeswa alishika nafasi ya nne na nafasi ya tano ilichukuliwa na Lengarusi Tpasoi wa Shule ya Sekondari Nanja.

Mkurugenzi Mtendaji wa Holili Youth Athletics Club, Domician Genandi alisema anafurahi kuona chipukizi aliowaandaa wanafanya vizuri katika medani ya riadha katika michuano hiyo.

Genandi aliongeza kusema Sokoine Min Marathon inaweza kuinua vipaji vya riadha kuanzia shule za msingi hasa ikizingatia kulionekana vipaji vizuri vya mbio hizo, ambavyo vikitafutiwa mazingira vinaweza kuing’arisha medani ya  riadha nchini.

Hata hivyo alitaka mbio za Sokoine Min Marathon zitengewe siku yake ili kuleta ladha zaidi hususani kwa masuala ya kiuchumi watu wa eneo hilo waweze kufanya biashara zao kwa uhuru hasa ikizingatiwa kwamba “Sokoine Day” hutawaliwa na shughuli nyingi za kisiasa.

Itakumbukwa kwamba Hayati Edward Moringe Sokoine alizaliwa Agosti 1, 1938 Kilasho Kijiji cha Emairete Monduli Juu mkoani Arusha kwa wazazi wake Baba Sokoine Ole Severe na Mama Napelel Sinyati Noomoyaki.

Sokoine Min Marathon 2014 Kilometa 2

Kilometa 2, kwa wanafunzi wa Shule za Msingi, Wasichana Nawasa Kamoyo(Euyati) alishika nafasi ya kwanza akifuatiwa na Patricia Leliel (Mazoezi), na nafasi ya tatu ikinyakuliwa na Neiyo Simon kutoka Shule ya Msingi Euyati.

Wavulana waliokimbia kilometa 2 na kushika nafasi tatu za kwanza walikuwa Kibori Jackson (Monduli Juu),  Emmanuel Clakoi (Monduli Juu)  na Paulo Leken (Monduli Juu).


Kilometa 10


WANAUME


1
Fabian Joseph

34:28.04
WNS
2
Alphonce Felix

34:45.39
HYAC
3
Dickson Marwa

34:57.47
HYAC
4
Gabriel Gerald

34:59.09
WNS
5
Fabian Nelson

35:07.20
CCP
 


WANAWAKE


1
Jackline Sakilu

40:01.26
JWTZ
2
Nathalia Elisante

40:51.27
ARUSHA
3
Failuna Abdi

41:13.54
WNS
4
Mary Naali

41:25.15
AAAC
5
Serina Amosi

43:24.70
ZANZIBAR
6
Flora Yuda

44:52.99
JWTZ



 
 

April 12, 2014; Mwanariadha chipukizi Adelina Audax (HYAC) aliibuka kidedea katika mbio za kuadhimisha miaka 30 tangu kifo cha Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine.


Adelina alitwaa taji la Sokoine Min Marathon kilometa 2 kwa upande wa wasichana katika ardhi ya Monduli Juu mkoani Arusha, mahali alipozaliwa Waziri huyo.

Adelina Audax anayetunzwa na Holili Youth Athletics Club katika kambi ya mazoezi ya klabu hiyo iliyopo Tarakea wilayani Rombo aliwaongoza wasichana wenzake kutoka klabu hapo Neema Mathias na Lidiuna Godfrey alishika nafasi ya tatu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete alimkabidhi taji la ushindi mbele ya viongozi wengi wa kisiasa na kidini waliohudhuria maadhimisho ya kifo cha Waziri Mkuu wa Zamani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Edward Sokoine.

Hayati Sokoine alifariki dunia Aprili 12, 1984 kwa ajali ya gari, mkoani Dodoma.




Leo katika “BIOGRAPHY CHAMBER” tumekueandalia Historia ya Mwanzilishi wa Klabu ya Riadha ya Holili (HYAC), Domician Genandi.

DOMICIAN GENANDI NI NANI?
Jina lake ni Domician Genandi Rwezaura (47), alizaliwa Desemba 29, 1967 katika kijiji cha Kagondo Wilayani Muleba mkoani Kagera.


Elimu ya Msingi aliipata katika Shule ya Msingi Kableme kijijini hapo kati ya mwaka 1980-1987. akafanikiwa kuendelea na masomo ya sekondari kati ya mwaka 1988-1992 (O-level) na 1993-1995 (A-level) katika Seminari ya Kikatoliki ya Uhuru iliyoko mkoani Kilimanjaro.

Kutokana na wito wake wa kuwa mtumishi wa kanisa la Katoliki (Upadre) aliamua kwenda kusomea masomo ya Falsafa katika Chuo cha Kanisa hilo kilichopo Nairobi (CUEA-Catholic University of East Africa) kati ya mwaka 1996-1999, Advanced Diploma of Philosophy. Aliachana na masuala ya wito katika kanisa hilo baada ya kumaliza mafunzo hayo ya miaka mitatu (3) mara baada ya kugundua anatakiwa aitumikie jamii akiwa ameoa.

Itakumbukwa kwamba Upadre katika Kanisa la Katoliki humtaka anayesomea wito huo asahau kabisa suala la kuwa na familia, hivyo kwa Domician lilikuwa ni suala gumu mno katika maisha yake. Alipotoka Nairobi alirudi mkoani Kilimanjaro na kuanza maisha yake katika eneo moja mkoani humo linalijulikana kwa jina la KIA akiwa na familia moja wazawa wa Lindi ambao walimlea na kumshawishi asomee masuala ya Utalii katika chuo kimoja mjini Arusha, hiyo ilikuwa mwaka 2000-2001 alipochukua Masomo ya Utalii, Ngazi ya Cheti (Tour Guide).

Akiwa mjini Arusha alikuwa akisoma masomo ya mbali ya Bussiness Administration katika ngazi ya Stashahada yaliyokuwa yakitolewa na chuo kimoja nchini Uingereza. Mwaka 2001 aliingia mjini Holili na kuanza masuala ya “Clearing & Forwading”, na baadaye kupata wazo la kuanzisha Klabu ya Riadha. Ikumbukwe kwamba wazazi wake walifariki akiwa darasa la tano (5) hiyo ilikuwa mwaka 1984.
Familia ya Domician Genandi, Februari 28, 2014; Holili-Rombo


Domician Genandi ana watoto watatu Winfrida (2003), Karen (2006) na Genandi (2009) akiwa na mkewe waliyefunga naye ndoa Julai 21, 2003.

Imetayarishwa na:
Jabir Johnson, Afisa Habari Holili Youth Athletics Club
Mei 2014.

No comments:

Post a Comment