HYAC

Attack with Style, Defend with Heart

Monday 12 May 2014

ELIBARIKI BUKO, ANDREW BONIFACE, FURAHA SAMBEKE WATISHA MBIO DAR



Jabir Johnson,
Afisa Habari HYAC akimvisha medali mshiriki.
Klabu ya riadha ya Holili Youth Athletics Club (HYAC) na Sekondari ya Makongo, ziling’ara katika mbio za majaribio mwishoni mwa juma kuandaa timu ya taifa zilizofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Wanariadha Stumai Abdallah, Adelina Trazius, Stella Chacha, Oprah Clement, na Sheldah Boniface kutoka Makongo, walichomoza katika mbio za mita 100; 200; 400 na 800 kwa upande wa wasichana.

Andrew Boniface, Elibariki Buko na Furaha Sambeke walioiwakilisha HYAC katika mbio za mita 400, 800, 1,500 na 3,000 walishika nafasi za juu.

Shelda Boniface ambaye pia ni mwanasoka anayechezea timu ya taifa ya chini ya miaka 20, Tanzanite na Stumai Abdallah walikimbia mita 100, wakitwaa nafasi ya kwanza na ya pili kwa muda wa  sekunde 12.32 na 12.79.

Katika mita 200, Stumai alishika nafasi ya kwanza akikimbia kwa muda wa sekunde 27.47 akifuatiwa na Adelina Trazius aliyetumia muda wa sekunde 27.93.

Stella Chacha na Oprah Clement walishika nafasi ya kwanza na ya tatu katika mita 800 huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Irene Chima (HYAC) wakikimbia kwa muda wa dakika 2:30.92, 2:42.40 na 2:51.35.

Kwa upande wa Andrew Boniface, aling’ara zaidi katika mita 200 (sekunde 22.40), mita 400 (sekunde 50.95); Elibariki Buko mita 800 (dakika 1:57.36), mita 1500 (dakika 3:58.51) na Furaha Sambeke aliibuka kidedea katika mita 3,000 akitumia muda wa dakika 9:31.27.
 
Akizungumza baada ya mbio hizo, Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam, Zainab Mbiro, aliwataka wadau wa michezo kujitokeza kwa wingi kudhamini majaribio hayo kwa ajili ya kuandaa timu ya taifa.

Alisema licha ya juhudi kubwa ya kutafuta wadhamini kwa lengo la kukuza kiwango cha mchezo huo, hadi sasa  hawana wadhamini, hivyo akatoa wito kwa makampuni na mashirika mbalimbali kuwekeza katika mchezo huo.

No comments:

Post a Comment