HYAC

Attack with Style, Defend with Heart

Friday 29 August 2014

KAMBI YA MAZOEZI YA HYAC YAHAMISHIWA HOLILI




 Adelina Audax, Furaha Sambeke na Ludwina Godfrey, baada ya kumaliza mazoezi ya asubuhi katika barabara za mji mdogo wa Holili uliopo mpakani mwa Tanzania na Kenya.

Wednesday 27 August 2014

GENANDI AHUDHURIA MKUTANO WA MAANDALIZI KILIMANJARO FESTIVAL 2014

 Mkurgenzi wa Holili Youth Athletics Club (wa kwanza kushoto) akiwasili katika Ukumbi wa Mikutano uliopo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Leonidas Gama, Nelson Brighton (Operation Manager HYAC) na Kiwango









Friday 22 August 2014

KONA YA PRO, JULAI 2014: NUTRITION FOR ATHLETES IS THE BIGGEST CHALLENGE TO THEIR PERFOMANCE



AFYA NA RIADHA
Diet, like the word “nutrition”, means all the food a person eats and drinks. Diet directly affects the performance and health of each athlete.  Coaches should be aware  that athletes’s eating and drinking patterns will influence how well they can train and whether they are able to complete at their best.

Coaches should work with athletes to develop healthy diets where they are individually aware of their personal nutritional goals and of how they can select the nutrition to meet these goals.

A well chosen diet offers many benefits to all athletes, regardless of event, gender, age or level of competition. These benefits include:

a.      Optimal gains from the training programme.
b.      Enhanced recovery within and between training sessions and competitions.
c.       Achievement and maintenance of an optimum body weight and physique.
d.      A reduced risk of injury and illness.
e.      Confidence in being well prepared for competition.
f.        Enjoyment  of food and social eating situations.

Despite these advantages many athletes do not meet their nutritional goals. The reasons for this can include:
a.      Poor knowledge of foods and drinks
b.      Coaches having poor or outdated knowledge of sports nutrition
c.       Poor choices when buying food
d.      Inadequate cooking skills
e.      Inadequate finances
f.        A busy lifestyle leading to inadequate time to obtain, prepare or consume appropriate foods
g.      Poor availability of good and drink choices
h.     Frequent travel
i.        Indiscriminate and incorrect use of supplements and sports food.

Next time we will look at the way food can play a very important part in successful training and competition. We will look at why the body needs food, which sorts of food are good for us, which are unnecessary and which are not so good and why. But first we should understand what we mean by “nutrition”.

NUTRITION means all the food a person eats  and drinks. The whole human body is made from this food, and all energy comes from food. The food acts in the body as a fuel, providing energy and chemicals for movements growth and keep the body healthy. What we need nutritionally  is affected by our age, gender, physique, level of physical activity and state of health.
Prepared by:
Jabir Johnson
Blogger & Photo Journalist
+255-(0)-768 096 793

Wednesday 20 August 2014

KONA YA PRO, JULAI 2014: B'E BRAZUCA NA JUMUIYA MADOLA ZASHANGAZA DUNIA



B’E
Katika kipengele hiki tutaangazia matukio makubwa yaliyotukia kwenye mwezi  Julai mwaka huu ambapo tumeshuhudia Kombe la Dunia nchini Brazil na Michuano ya Jumuiya Madola ikirindima jijini Glasgow nchini Scotland.

Kombe la Dunia 2014 Brazil
Lilianza Juni 12 kwa kutumia mpira uliopachikwa jina la Brazuca, kwa wenyeji Brazil kufungua dimba dhidi ya Croatia ambapo walishinda mabao 3-1, ikiwa ni mtanange wa kundi A. 

Marcelo Viera aliweka rekodi ya kuwa wa kwanza kufumania nyavu alipojifunga hivyo kuwa mchezaji wa kwanza tangu Kombe la Dunia lianzishwe mwaka 1930, kujifunga kwa timu mwenyeji.

Aidha katika Kombe hilo kulishuhudiwa bingwa mtetezi Hispania akipokea kichapo cha mabao 5-1 kutoka Uholanzi, kisha 2-0 kutoka Chile na kuondolewa licha ya kushinda 3-0 dhidi ya Australia.

Hata hivyo haikuishia hapo kichapo cha mabao 7-1 ilichopokea Brazil kutoka kwa Ujerumani katika Kombe hilo ndicho kilichoacha gumzo kubwa kwani haijawahi kutokea katika hatua ya nusu fainali.

Pia timu za barani Afrika ambazo ni Cameroon, Algeria, Ghana, Nigeria na Ivory Coast zilijitahidi kucheza mchezo wa kuvutia licha ya kutofika mbali.

Algeria na Nigeria ndizo pekee zilizonusa hatua ya 16 bora baada ya kutoka katika hatua ya makundi (32). Algeria ilipambana na Ujerumani wakati Nigeria ikitoana jasho na Ufaransa.

Fainali ilichezwa katika uga wa Maracana Jijini Rio De Janeiro kati ya Ujerumani na Argentina ambapo Ujerumani (Die Mannschafts) ikivunja rekodi kwa kulinyakua kwa mara ya kwanza kutoka ardhi ya Amerika ya Kusini kwa kuizaba Albicelestes kwa bao 1-0 lilifungwa katika dakika ya 114 na Mario Gotze akitokea benchi.

Kubwa zaidi Miroslav Klose (Ujerumani) alivunja rekodi kwa kuwa mfungaji mwenye mabao mengi ya Kombe la Dunia akifikisha 17 na kuvunja rekodi ya Ronaldo de Lima aliyefunga mabao 15.

Kiatu cha dhahabu kilikwenda kwa nyota kutoka Colombia, James Rodriguez aliyetupia mabao 6 katika michuano hiyo iliwanyima raha wabrazil wakimaliza kwa kichapo cha mabao 3-0 kutoka Uholanzi.

Michuano ya Jumuiya ya Madola, Glasgow-Scotland
Maajabu hutokea kwani shilingi ni ndogo inazama kwenye maji lakini meli ni kubwa haizami; michuano ya Jumuiya ya Madola ilianza siku 10 baada ya kumalizika kwa Kombe la Dunia nchini Brazil yaani Julai 23 katika Jiji la Glasgow nchini Scotland.

Michuano hii hushirikisha nchi ambazo zilitawaliwa na Mwingereza katika medani ya michezo, hivyo michezo mbalimbali huwepo katika michuano hiyo Judo, riadha, ngumi za ridhaa, kuogolea, mpira wa meza na kadhalika.

Tanzania imeambulia patupu katika michezo mitano iliyoenda kuwakilisha katika michuano hiyo huko ughaibuni, wakati nchi jirani ya Kenya imetwaa medali 25 huku England ikiongoza kwa kuwa na medali nyingi.

Michuano hiyo imefungwa Agosti 3, mwaka huu kukishuhudia vifijo na nderemo vikipigwa katika Jiji la Glasgow.

Mkimbiaji anayeshikilia rekodi ya dunia ya kasi Usain Bolt siku ya Jumamosi ya Agosti 2 alitwaa medali ya dhahabu katika mbio za relay 4×400.

Bolt alimkung’uta Mwingereza Danny Talbot aliyemaliza wa pili akikimbia kwa sekunde 37.58 huku Talbot akimaliza kwa sekunde 38.02

Bolt anajiandaa na mbio za Diamond IAAF za Agosti 28 katika uga wa Lepzig ambako anatarajiwa kuwa tishio zaidi.

Huku Danny Talbot akijiweka katika matumaini makubwa ya kunyakua medali katika Michuano ya Ubingwa wa Ulaya itakayofanyika baadaye mwezi ujao.

Haya ni matukio makubwa mawili yaliyojiri mwezi Julai na kukonga nyoyo za mashabiki duniani.
Prepared by:
Jabir Johnson
Blogger & Photo Journalist
+255-(0)-768 096 793

Sunday 17 August 2014

KONA YA PRO, JULAI 2014: OTTO SEKI ATISHA



SURPRISE RIO
Leo tutamwangazia mwanariadha Ottoman Seki.




Hebu tazama picha hizi, utafurahi tu.

Katika rekodi ya mbio alikimbia Kili Marathon 2013 kilometa 5, na Mt. Kilimanjaro Marathon 2014 kilometa 10.

Katika mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon 2014 alishika nafasi ya pili kwa kutumia muda wa saa 1:14.20 akitanguliwa na Hilary Hendry kwa muda wa saa 1:08.10

Otto kama ambavyo amekuwa akijulikana na wengi alisoma Elimu yake Msingi katika Misheni ya Potwe-Ndondondo wilayani Muheza kuanzia mwaka 1984-1991.



Ottoman Seki ndio Surprise Rio wa mwezi wa 7.

Prepared by:
Jabir Johnson
Blogger & Photo Journalist
+255-(0)-768 096 793