HYAC

Attack with Style, Defend with Heart

Sunday 17 August 2014

CAREN AND GENANDI WISHES PRO J, HAPPY BIRTHDAY



Caren na mdogo wake Genandi, wote wakiwa ni watoto wa Domician Genandi Rwezaura ambaye ni Mkurugenzi wa Holili Youth Athletics Club (HYAC) iliyopo wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro wamesheherekea kutimiza miaka 30 ya Afisa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo Jabir Johnson.

Hafla hiyo fupi imefanyika katika Kijiji cha Holili kilichopo mpakani mwa Tanzania na Kenya katika mpaka wa Taveta/Holili mapema leo asubuhi ambapo Caren na Genandi wamempa picha kubwa waliyompiga hivi karibuni ikiwa ni ukumbusho wake wa kutimiza miaka 30 ya kuzaliwa kwake.

Afisa Habari na Mawasiliano huyo ameishukuru sana familia ya mkurugenzi huyo pamoja na wafanyakazi na wachezaji wa klabu hiyo kwa kumtakia maisha mema na yenye baraka tele kwa maendeleo ya taifa kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment