HYAC

Attack with Style, Defend with Heart

Sunday 27 July 2014

GENANDI AHUDHURIA MSIBA WA NGULI WA HABARI ZA MICHEZO, KIPESE



Mkurugenzi wa Holili Youth Athletics Club (HYAC), Domician Genandi amehudhuria msiba wa mwandishi habari na mtangazaji wa michezo Hafidh Henry Lyimo aliyefariki kwa ajali jana usiku, maeneo ya Mfulie barabara ya Mwika akitokea Rombo katika shughuli zake.
 




Genandi aliwasili majira ya saa 10 jioni maeneo ya National House (NHC) mjini Moshi ulipo msiba wa mtangazaji huyo, ambaye alikuwa mdau mkubwa wa HYAC.

Mkurugenzi huyo alisema amepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha mdau mkubwa ambaye jamii ya Tanzania haitamsahau kamwe kutokana na mchango wake katika uga wa michezo.

Hata hivyo alito pole kwa wafiwa kwa tukio hilo la kusikitisha na akuongeza kuwa Mwenyezi Mungu aweze kuwashikilia wafiwa hao katika kipindi hiki kigumu.

Mwili wa marehemu utazikwa katika makaburi ya Soweto mjini Moshi Julai 28, mwaka huu.

PREVIOUS CHAMBER

KIPESE, A RADIO PRESENTER IN MOSHI, IS NO MORE



Tasnia ya Habari na wanamichezo mkoani Kilimanjaro imepata pigo kufuatia kifo cha ghafla cha Mtangazaji wa kituo cha redio Moshi FM Hafidh Henry Lyimo “Kipese” .
Kipese amefariki dunia usiku wa jana majira ya saa 2 akiwa njiani akitokea Rombo katika eneo la makutano ya barabara ya Mwika baada ya pikipiki aliyokuwa akitumia kugongana na pikipiki nyingine.

Taarifa za awali zinasema Marehemu Kipese alikuwa akitokea wilayani Rombo ambako amekuwa akifanya shughuli zake na kwamba wakati anarejea ndipo mauti yakamfika baada ya kuumia vibaya katika ajali hiyo.

Kipese alikuwa katika pikipiki aina ya Toyo yenye namba za usajili T 115 CAU

Katika hatua ya kwanza mwili wa marehemu ulihifadhiwa katika hospitali ya Kilema wilayani Moshi vijijini  kungojea taratibu nyingine toka kwa ndugu zake ambapo Julai 27 mwaka huu mwili huo ulihamishiwa katika Hospitali ya KCMC mjini Moshi.

Tayari makundi mbalimbali ambayo marehemu amekuwa karibu nayo kwa shughuli za kikazi yametoa taarifa za masikitiko kufuatia kifo cha Kipese.

Makundi hayo ni Wanahabari mkoani Kilimanjaro, Vyama vya Michezo mkoani humo kikiwemo KRFA, na  wadau wa michezo mkoani Kilimanjaro ambako licha ya kwamba Marehemu Kipese alikuwa mtangazaji wa kipindi cha Michezo katika redio aliyokuwa akifanyia kazi pia alikuwa mwamuzi wa mchezo wa soka.

Safari ya mwisho ya Marehemu Hafidh Lyimo itakuwa kesho (Julai 28, mwaka huu)  katika makaburi ya Soweto mjini Moshi

PREVIOUS CHAMBER



CHANZO: JAIZMELALEO

Thursday 24 July 2014

AFRICAN FOOD: PASTA PARTY, A DAY BEFORE MT. KILIMANJARO MARATHON 2014



A day before Mt. Kilimanjaro Marathon 2014 was very brilliant day in Moshi.



This was June 29, 2014 at Moshi Club

Guests from United States of America (USA), Republic of Ireland and Tanzanians participated in “get together party”.

Most interesting was the present of Music Band called “Clarinet For Conservation” you know why, I will tell you later.

The present of Assistant Commissioner  of Kilimanjaro Regional Mr.Estomih Makyara was most remarkable point in that event.

The Director and Founder of Mt. Kilimanjaro Marathon Marie Frances, invited all the guests in the party was wonderful day!

Let’s have a look on:          
Food
Famous Snacks: maandazi (fried dough), isheti, kashata, kebab (kabaab), samosa (sambusa), mkate wa kumimina (Zanzibar rice bread), vileja, vitumbua (rice patties), bagia, and many others.

Along the coastal regions (Dar es Salaam, Tanga, Bagamoyo, Zanzibar, and Pemba), spicy foods are common, and there is also much use of coconut milk. Regions in Tanzania's mainland also have their own unique foods. Some typical mainland Tanzanian foods include rice (wali), ugali (maize porridge), chapati (a kind of bread), nyama choma (grilled meat), mshikaki (marinated beef), fish, pilau, biryani, and ndizi-nyama (plantains with meat). Commonly used vegetables include bamia (okra), mchicha (a kind of spinach), njegere (green peas), maharage (beans), and kisamvu (cassava leaves).
Many people drink tea (chai) in Tanzania. Usually tea is drunk in the morning, during breakfast with chapati and maandazi, and at times at night during supper. Coffee is second, and is usually taken in the evening, when the sun is down, and people are on the front porch, playing cards or bao. Many people drink coffee with kashata (a very sweet tasting snack made from coconut meat or groundnuts).

Prepared by;
Jabir Johnson,
Blogger and Photo Journalist,

Tuesday 15 July 2014

RAIS KIKWETE AKABIDHI BENDERA, TIMU YA TAIFA, JUMUIYA YA MADOLA



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhi bendera ya taifa kwa Suleiman Kidunda mkuu wa msafara wa timu itakayokwenda Jumuiya ya Madola Julai 16, mwaka huu; katikati ni Muharami Mchume.

Mwenyekiti wa TOC, Filbert Bayi akizungumza jambo.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza jambo.
Rais Kikwete akikagua Uwanja wa Taifa
Rais Kikwete katika picha ya pamoja

CHANZO: FRANCIS DANDE