HYAC

Attack with Style, Defend with Heart

Sunday 27 July 2014

GENANDI AHUDHURIA MSIBA WA NGULI WA HABARI ZA MICHEZO, KIPESE



Mkurugenzi wa Holili Youth Athletics Club (HYAC), Domician Genandi amehudhuria msiba wa mwandishi habari na mtangazaji wa michezo Hafidh Henry Lyimo aliyefariki kwa ajali jana usiku, maeneo ya Mfulie barabara ya Mwika akitokea Rombo katika shughuli zake.
 




Genandi aliwasili majira ya saa 10 jioni maeneo ya National House (NHC) mjini Moshi ulipo msiba wa mtangazaji huyo, ambaye alikuwa mdau mkubwa wa HYAC.

Mkurugenzi huyo alisema amepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha mdau mkubwa ambaye jamii ya Tanzania haitamsahau kamwe kutokana na mchango wake katika uga wa michezo.

Hata hivyo alito pole kwa wafiwa kwa tukio hilo la kusikitisha na akuongeza kuwa Mwenyezi Mungu aweze kuwashikilia wafiwa hao katika kipindi hiki kigumu.

Mwili wa marehemu utazikwa katika makaburi ya Soweto mjini Moshi Julai 28, mwaka huu.

PREVIOUS CHAMBER

No comments:

Post a Comment