HYAC

Attack with Style, Defend with Heart

Sunday 27 July 2014

KIPESE, A RADIO PRESENTER IN MOSHI, IS NO MORE



Tasnia ya Habari na wanamichezo mkoani Kilimanjaro imepata pigo kufuatia kifo cha ghafla cha Mtangazaji wa kituo cha redio Moshi FM Hafidh Henry Lyimo “Kipese” .
Kipese amefariki dunia usiku wa jana majira ya saa 2 akiwa njiani akitokea Rombo katika eneo la makutano ya barabara ya Mwika baada ya pikipiki aliyokuwa akitumia kugongana na pikipiki nyingine.

Taarifa za awali zinasema Marehemu Kipese alikuwa akitokea wilayani Rombo ambako amekuwa akifanya shughuli zake na kwamba wakati anarejea ndipo mauti yakamfika baada ya kuumia vibaya katika ajali hiyo.

Kipese alikuwa katika pikipiki aina ya Toyo yenye namba za usajili T 115 CAU

Katika hatua ya kwanza mwili wa marehemu ulihifadhiwa katika hospitali ya Kilema wilayani Moshi vijijini  kungojea taratibu nyingine toka kwa ndugu zake ambapo Julai 27 mwaka huu mwili huo ulihamishiwa katika Hospitali ya KCMC mjini Moshi.

Tayari makundi mbalimbali ambayo marehemu amekuwa karibu nayo kwa shughuli za kikazi yametoa taarifa za masikitiko kufuatia kifo cha Kipese.

Makundi hayo ni Wanahabari mkoani Kilimanjaro, Vyama vya Michezo mkoani humo kikiwemo KRFA, na  wadau wa michezo mkoani Kilimanjaro ambako licha ya kwamba Marehemu Kipese alikuwa mtangazaji wa kipindi cha Michezo katika redio aliyokuwa akifanyia kazi pia alikuwa mwamuzi wa mchezo wa soka.

Safari ya mwisho ya Marehemu Hafidh Lyimo itakuwa kesho (Julai 28, mwaka huu)  katika makaburi ya Soweto mjini Moshi

PREVIOUS CHAMBER



CHANZO: JAIZMELALEO

No comments:

Post a Comment