Julai 2014
Yaliyomo
- UTANGULIZI
- HOLILI YOUTH ATHLETICS CLUB
- UNAWAKUMBUKA?
- AFYA NA RIADHA
- SURPRISE RIO!
- B’E
- TO THE BEST
- BIOGRAPHY CHAMBER
UTANGULIZI
Baada ya pilikapilika za
Kombe la Dunia nchini Brazil mwezi Juni na Julai mwaka huu sasa tumekutana tena
huku tukiwa na mengi ya kuzungumza katika Utangulizi wetu kwenye toleo hili.
Michuano ya Jumuiya ya
Madola imemalizika katika Jiji la Glasgow nchini Scotland huku watanzania
tukiishia patupu katika michezo mitano iliyokwenda kutuwakilisha.
Nijikite katika mchezo
wa riadha, ambao umetupa masikitiko makubwa, kwani tulijua kwamba hatutachukua
medali yoyote kutokana na mfumo wa uteuzi wa wachezaji wetu.
Kubwa zaidi tusahau
yaliyopita kwani viongozi wetu wamerudi wakiwa vichwa chini kutokana na
wachezaji waliowateua kuiwakilisha
Tanzania katika michuano hiyo kufanya vibaya.
Licha ya kwenda na
kurudi bila medali yoyote lakini ninajua wazi kuwa kuna mambo viongozi wetu wa
Chama cha Riadha (RT) na Kamati ya Olimpiki (TOC) watakuwa wamejifunza huko,
rai yangu kwao ni kwamba mambo hayo mazuri waliyoyaona na kuyapata huko
wawarudishie watanzania kwani “kuvunjika
kwa koleo sio mwisho wa uhunzi”.
Wachezaji hawatakiwi
hata kidogo kuacha kufanya mazoezi kwani itatugharimu zaidi katika michuano
ijayo, hivyo basi ni wazi kujifunza na kurekebisha pale tulipokosea ili kutulia
katika msemo usema “Don’t live in the
past, Learn from it…”
Nikutakie utendaji mwema
wa majukumu yako kwa mwezi Agosti.
Domician
Genandi
Mkurugenzi
Mtendaji
Holili Youth
Athletics Club (HYAC)
Julai 2014.
No comments:
Post a Comment