HYAC

Attack with Style, Defend with Heart

Friday 29 November 2013

DICKSON MARWA KUONGOZA UHURU MARATHON



http://www.apb.se/preview/070827_2909.jpgMWANARIADHA mahiri, Dickson Marwa, anatarajiwa kuwaongoza wanariadha wengine 10 kuipeperusha bendera ya Klabu ya Riadha ya Holili, ‘Holili Youth Athletic Club (HYAC)’, kwenye mbio za kwanza za Uhuru Marathon zitakazotimua vumbi Desemba 8 jijini Dar es Salaam.

Dickson ambaye kwa sasa ni moto wa kuotea mbali katika mbio za kilomita 21 (Nusu Marathon), atawaongoza wenzake Nelson Priva, Alfonce Felix, Saidi Makula, Lucian Reginald, Catherine Lange, Fadhila Salum, Consolata Samwel, Selina Amos na Augustino Sulle katika kilomita 21 pamoja na Dotto Ikangaa atakayeshiriki kilomita 5.

Mkurugenzi mtendaji wa klabu hiyo, Domician Rwezaura, katika mahojiano maalumu ofisini kwake alisema kwamba Marwa na wenzake wataondoka Desemba 7 wakiongozana na viongozi wanne akiwemo kocha wao, Adram Mikumi, Meneja Nelson Mrashani, na Katibu Innocent pamoja na mwenyewe.

Rwezaura alisema, mazoezi yanaendelea katika kambi ya mazoezi yaliyoko Tarakea.

Wakati huohuo, fomu za usajili wa mbio za Uhuru Marathon zimeanza kutolewa siku ya Jumapili  katika ofisi za klabu ya Holili zilizoko katika jengo la Plaza, mkabala na stendi ndogo ya mabasi ya mjini Moshi.

No comments:

Post a Comment