HYAC

Attack with Style, Defend with Heart

Monday 7 April 2014

KAMATI YA MAANDALIZI SOKOINE MIN MARATHON YAOMBA RADHI WADAU



Kamati ya maandali ya Sokoine Min Marathon 2014 imeomba radhi kwa wanariadha na wadau wa mchezo huo nchini, kuwa imebadilisha badala ya kilometa 21 wameiweka kilometa 10.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Wilhem Gidabuday alisema kubadilisha kwa mbio hizo kumetokana na ukweli kwamba mbio hiyo inafuatana na mbio nyingine juma moja baadaye hivyo itakuwa ni vigumu kwa wanariadha kuhudhuria pande zote mbili.

TAARIFA YAKE KWA VYOMBO VYA HABARI
Tunaomba radhi kwa kufanya mabadiliko ya ghafla! Hiyo ni kutokana na mashauriano kati yetu sisi waandaaji, Chama Cha Riadha Mkoa  na wanariadha wenyewe.

SABABU KUU: Imeamuliwa kwamba siyo vizuri kuwakimbiza wanariadha mbio ndefu mara mbili kwa wiki moja sababu pia kutakuwa na Ngorongoro Half Marathon April 19, 2014.

Familia imeridhia ombi letu na pia imekuwa wazo zuri kwa wanariadha wazoefu ambao wanafahamu athari za kukimbia mbio ndefu mfululizo. Pia wananchi wengi sasa wataweza kushiriki Kilomita 10.


Taratibu zingine hadi sasa zipo kama ilivyopangwa, ila namba zinasajiliwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Karume. Tsh: 2,000 tu kwa kusajili namba yako. ZAWADI ZITATOLEWA KWA WASHINDI.

No comments:

Post a Comment