HYAC

Attack with Style, Defend with Heart

Wednesday 26 March 2014

NELSON MRASHAN AHITIMU MAFUNZO YA UKOCHA RIADHA TANZANIA


NELSON MRASHANI

Nelson Brighton Mrashan ni miongoni mwa makocha wa mchezo wa Riadha waliohitimu mafunzo ya ukocha ngazi ya pili ya cheti.

Nelson Mrashan alihitimu mafunzo hayo Machi 28, mwaka huu, yaliyochukua majuma mawili kuanzia Machi 15 hadi 28 mwaka huu Mjini Kibaha.

Akizungumza baada ya kuhitimu mafunzo Mrashan alisema huo ni mwanzo mzuri katika kuinua mchezo wa riadha nchini Tanzania.

Chama cha Riadha nchini kimetoa shukrani zake za dhati kwa Holili Youth Athletics Club (HYAC) kuwa mbele katika kuinua mchezo wa riadha hasa ikizingatiwa kuwa Nelson Mrashan ni Operation Manager wa klabu hiyo.

RT kupitia barua yake kwa HYAC ya Machi 28 mwaka huu ilisema wahitmu wa mafunzo hayo wanapaswa kupewa kipaumbele katika kutambuliwa kwao ili waweze kutoa taaluma waliyoipata na sio kukaa na vyeti bila kuwajibika
WAHITIMU WA MAFUNZO YA UKOCHA MJINI KIBAHA MACHI 28, 2014


1 comment:

  1. Haya makocha hao tumewafundisha na wako tayari kufanya kazi yao.

    Sasa kwa nini tuajiri makocha kutoka nchi za nje na makocha wetu wapo ??

    ReplyDelete