HYAC

Attack with Style, Defend with Heart

Saturday 1 March 2014

SUPERSPORT WAZURU HOLILI YOUTH ATHLETICS CLUB



Holili Youth Athletics Club (HYAC) ya mkoani Kilimanjaro imepata ugeni kutoka Afrika Kusini huku ikiajiandaa na ushiriki wake Kili Marathon 2014.
 
DEBBIE HARRISON, DOMICIAN GENANDI NA PAUL RAILTON
Ugeni kutoka nchini Afrika Kusini umeongozwa na Deborah Harrison mwandaaji wa Kili Marathonmbio zilizo kivutio nchini Tanzania.


DOMICIAN GENANDI AKITOA MAELEZO KWA WAGENI KUTOKA AFRIKA KUSINI
Debbie Harrison kama ambavyo amekuwa akitumia aliwasili katika Ofisi za HYAC mjini Holili, mpaka mwa Tanzania na Kenya majira ya saa 5:20 asubuhi akiwa na Mpiga Picha kutoka SuperSport Paul Railton na kupokewa na Mkurugenzi Mtendaji wa klabu hiyo ya riadha Domician R. Genandi .

Debbie alisema amekuwa akiratibu mbio za Kili Marathon kwa muda mrefu sasa lakini hakuwa amewahi kusikia kama kuna klabu ya riadha mkoani Kilimanjaro yenye kambi yake Tarakea wilayani Rombo.

Aliongeza kusema kitendo kilichofanywa na HYAC ni cha kuigwa nchini Tanzania kwa ajili ya kuinua riadha kwa ujumla wake.

Pia alisema kuwaweka kambi wachezaji wa riadha zaidi ya 15 ni la uzalendo zaidi kutokana na ukweli kwamba miaka ya nyuma Tanzania ilikuwa juu sana katika riadha.

Ujumbe huo kutoka Afrika Kusini ulitoka mjini Holili na kuelekea Tarakea kujionea Kambi ya wachezaji HYAC.
KUTOKA KUSHOTO OPERATION MANAGER NELSON MLASHANI, CEO DOMICIAN GENANDI, PRO JOHNSONJABIR, SUPERSPORT CORRESPONDENT PAUL RAILTON NA DEBBIE HARRISON; MSTARI WA MBELE WINFRIDA GENANDI, KUKUGONZA  GENANDI, KAREN GENANDI NA HYAC SECRETARY INNOCENT THOMAS

No comments:

Post a Comment