HYAC

Attack with Style, Defend with Heart

Tuesday 15 April 2014

ADELINA AUDAX ATWAA TAJI, SOKOINE MIN MARATHON 2K



MONDULI JUU: Adelina Audax, mwanariadha chipukizi wa Holili Youth Athletics Club (HYAC) kuchukua taji la mbio za Sokoine Min Marathon kilometa 2 kwa wasichana mwishoni mwa wiki.
ADELINA AUDAX
Sokoine Min Marathon ilifanyika Monduli Juu ikiwa ni Maadhimisho ya miaka 30 tangu kutokea kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Aprili 12, 1984 mkoani Dodoma.

Neema Mathias na Lidiuna Godfrey walinyakua nafasi za pili na tatu wote wakiwa ni wanariadha chipukizi kutoka HYAC, nafasi ya nne na tano zilichukuliwa na Susan Patrick (Bala Secondary School), Sofia Olodi (Okikeso Secondary School).

Kwa upande wa wavulana kilometa 2 Oshun Simon (Nanja Secondary School) alitwaa taji hilo; huku nafasi ya pili na tatu ikichukuliwa na vijana kutoka Shule ya Sekondari ya Moita ambao ni Kalei Mereso na Ngoyai Ormeki.

Sabero Naisike wa Shule ya Sekondari ya Orkeswa alishika nafasi ya nne na nafasi ya tano ilichukuliwa na Lengarusi Tpasoi wa Shule ya Sekondari Nanja.

Mkurugenzi Mtendaji wa Holili Youth Athletics Club, Domician Genandi alisema anafurahi kuona chipukizi aliowaandaa wanafanya vizuri katika medani ya riadha katika michuano hiyo.

Genandi aliongeza kusema Sokoine Min Marathon inaweza kuinua vipaji vya riadha kuanzia shule za msingi hasa ikizingatia kulionekana vipaji vizuri vya mbio hizo, ambavyo vikitafutiwa mazingira vinaweza kuing’arisha medani ya  riadha nchini.

Hata hivyo alitaka mbio za Sokoine Min Marathon zitengewe siku yake ili kuleta ladha zaidi hususani kwa masuala ya kiuchumi watu wa eneo hilo waweze kufanya biashara zao kwa uhuru hasa ikizingatiwa kwamba “Sokoine Day” hutawaliwa na shughuli nyingi za kisiasa.

Itakumbukwa kwamba Hayati Edward Moringe Sokoine alizaliwa Agosti 1, 1938 Kilasho Kijiji cha Emairete Monduli Juu mkoani Arusha kwa wazazi wake Baba Sokoine Ole Severe na Mama Napelel Sinyati Noomoyaki.


No comments:

Post a Comment