Jabir Johnson,
Afisa Habari HYAC akimvisha medali
mshiriki.
|
Wanariadha
Stumai Abdallah, Adelina Trazius, Stella Chacha, Oprah Clement, na Sheldah
Boniface kutoka Makongo, walichomoza katika mbio za mita 100; 200; 400 na 800
kwa upande wa wasichana.
Andrew
Boniface, Elibariki Buko na Furaha Sambeke walioiwakilisha HYAC katika mbio za
mita 400, 800, 1,500 na 3,000 walishika nafasi za juu.
Shelda
Boniface ambaye pia ni mwanasoka anayechezea timu ya taifa ya chini ya miaka
20, Tanzanite na Stumai Abdallah walikimbia mita 100, wakitwaa nafasi ya kwanza
na ya pili kwa muda wa sekunde 12.32 na 12.79.
Katika
mita 200, Stumai alishika nafasi ya kwanza akikimbia kwa muda wa sekunde 27.47
akifuatiwa na Adelina Trazius aliyetumia muda wa sekunde 27.93.
Stella
Chacha na Oprah Clement walishika nafasi ya kwanza na ya tatu katika mita 800
huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Irene Chima (HYAC) wakikimbia kwa muda wa
dakika 2:30.92, 2:42.40 na 2:51.35.
Kwa
upande wa Andrew Boniface, aling’ara zaidi katika mita 200 (sekunde 22.40),
mita 400 (sekunde 50.95); Elibariki Buko mita 800 (dakika 1:57.36), mita 1500
(dakika 3:58.51) na Furaha Sambeke aliibuka kidedea katika mita 3,000 akitumia
muda wa dakika 9:31.27.
Akizungumza
baada ya mbio hizo, Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam,
Zainab Mbiro, aliwataka wadau wa michezo kujitokeza kwa wingi kudhamini
majaribio hayo kwa ajili ya kuandaa timu ya taifa.
Alisema
licha ya juhudi kubwa ya kutafuta wadhamini kwa lengo la kukuza kiwango cha
mchezo huo, hadi sasa hawana wadhamini, hivyo akatoa wito kwa makampuni
na mashirika mbalimbali kuwekeza katika mchezo huo.
No comments:
Post a Comment