HYAC

Attack with Style, Defend with Heart

Sunday, 17 August 2014

CAREN AND GENANDI WISHES PRO J, HAPPY BIRTHDAY



Caren na mdogo wake Genandi, wote wakiwa ni watoto wa Domician Genandi Rwezaura ambaye ni Mkurugenzi wa Holili Youth Athletics Club (HYAC) iliyopo wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro wamesheherekea kutimiza miaka 30 ya Afisa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo Jabir Johnson.

Hafla hiyo fupi imefanyika katika Kijiji cha Holili kilichopo mpakani mwa Tanzania na Kenya katika mpaka wa Taveta/Holili mapema leo asubuhi ambapo Caren na Genandi wamempa picha kubwa waliyompiga hivi karibuni ikiwa ni ukumbusho wake wa kutimiza miaka 30 ya kuzaliwa kwake.

Afisa Habari na Mawasiliano huyo ameishukuru sana familia ya mkurugenzi huyo pamoja na wafanyakazi na wachezaji wa klabu hiyo kwa kumtakia maisha mema na yenye baraka tele kwa maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Friday, 15 August 2014

KONA YA PRO, JULAI 2014: GENANDI AITAKA JAMII YA KITANZANIA KUJIPANGA MASHINDANO MAKUBWA YA RIADHA



 Julai 2014
Yaliyomo
  1. UTANGULIZI
  2. HOLILI YOUTH ATHLETICS CLUB
  3. UNAWAKUMBUKA?
  4. AFYA NA RIADHA
  5. SURPRISE RIO!
  6. B’E
  7. TO THE BEST
  8. BIOGRAPHY CHAMBER
UTANGULIZI
Baada ya pilikapilika za Kombe la Dunia nchini Brazil mwezi Juni na Julai mwaka huu sasa tumekutana tena huku tukiwa na mengi ya kuzungumza katika Utangulizi wetu kwenye toleo hili.

Michuano ya Jumuiya ya Madola imemalizika katika Jiji la Glasgow nchini Scotland huku watanzania tukiishia patupu katika michezo mitano iliyokwenda kutuwakilisha.

Nijikite katika mchezo wa riadha, ambao umetupa masikitiko makubwa, kwani tulijua kwamba hatutachukua medali yoyote kutokana na mfumo wa uteuzi wa wachezaji wetu.

Kubwa zaidi tusahau yaliyopita kwani viongozi wetu wamerudi wakiwa vichwa chini kutokana na wachezaji waliowateua  kuiwakilisha Tanzania katika michuano hiyo kufanya vibaya.

Licha ya kwenda na kurudi bila medali yoyote lakini ninajua wazi kuwa kuna mambo viongozi wetu wa Chama cha Riadha (RT) na Kamati ya Olimpiki (TOC) watakuwa wamejifunza huko, rai yangu kwao ni kwamba mambo hayo mazuri waliyoyaona na kuyapata huko wawarudishie watanzania kwani “kuvunjika kwa koleo sio mwisho wa uhunzi”.

Wachezaji hawatakiwi hata kidogo kuacha kufanya mazoezi kwani itatugharimu zaidi katika michuano ijayo, hivyo basi ni wazi kujifunza na kurekebisha pale tulipokosea ili kutulia katika msemo usema “Don’t live in the past, Learn from it…”

Nikutakie utendaji mwema wa majukumu yako kwa mwezi Agosti.
Domician Genandi
Mkurugenzi Mtendaji
Holili Youth Athletics Club (HYAC)
Julai 2014.

FOMU ZA KUJIUNGA NA HOLILI YOUTH ATHLETICS CLUB



 FOMU YA KUJIUNGA
1)     Jina la Mchezaji…………………………………………………..
2)    Umri wa Mchezaji………………………………………………..
3)    Alikozaliwa…………………………………………………………
4)    Uraia………………………………………………………………….
5)    Anakotokea kwa sasa:
Kijiji……………………………………………………………………
Kata……………………………………………………………………
Wilaya…………………………………………………………………
Mkoa…………………………………………………………………..

6)    Anuani……………………………………………………………………………………………………………………..
7)    Namba ya simu………………………………………………………………………………………………………
8)   Jina la Mlezi/Mdhamini…………………………………………………………………………………………
9)    Mawasiliano ya Mlezi/Mdhamini………………………………………………………………………..
10)           Afisa Michezo wa Wilaya/Mkoa…………………………………………………………………….
11) Una matatizo yoyote ya kiafya 
(thibitisha kupitia vyeti vya kidaktari na muhuri wa hospitali      husika)……………………………………………………………………………………………………………............................................................................................
12)            Historia yako ya riadha
    (Je, umewahi kushiriki mashindano yoyote?)
………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

 
MASHARTI YA HOLILI YOUTH ATHLETICS CLUB (HYAC)
Wajibu wa jumla wa mwanariadha
·         Kuheshimu haki, usawa na utu kwa kila mwanariadha, kocha, benchi la ufundi na wote wanaohusika katika klabu hii, usifanye upendeleo.
·         Unapaswa kuwa na maadili, kama mchezaji unapokuwa nje ya uwanja pia ndani ya riadha kwa ujumla.
·         Una wajibu wa kutoa ushirikiano kwa makocha, benchi la ufundi, mameneja wa timu, madaktari wa timu, wawakilishi wa klabu na viongozi wa nchi kwa faida ya mchezaji mwenyewe na klabu.
·         Unapaswa kuwa balozi mzuri unayejali kanuni za mchezo wa riadha, usiende kinyume nazo pia usitumie madawa yaliyokatazwa katika mchezo wa riadha.
·         Unapaswa kutoa taarifa kwa kocha wako, kuhusu maendeleo yako katika mazoezi kama yalivyopangwa kama kuna faida yoyote unayoipata au la.
·         Unapaswa kuwa na vifaa vya mchezo husika, tangu siku ya kwanza unapojiunga (kama ilivyoanishwa katika fomu hii), na ukisha kubaliwa unatakiwa kufuata ratiba ya klabu kwa wakati.
·         Mara zote toa shukrani kwa makocha na maafisa wengine wa klabu pindi unapokuwa katika mazoezi au michuano.
·         Epuka kutumia kauli mbaya, ikiwemo kuapa au kuwa na tabia hatarishi kwako na kwa wanariadha wengine, epukana na fujo, ugomvi na kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi na mwanariadha wa klabu.
·         Unapotaka kuhamia klabu nyingine ya riadha, taarifa ni lazima zifike katika ngazi ya utawala kwa maandishi ili kufikia makubaliano ya pande zote mbili.
·         Utakaporuhusiwa kujiunga na klabu utapewa sheria za jumla za kambi na kwenye michuano mbalimbali.

Mahitaji ya awali ya mwanariadha atakapokubaliwa maombi ya kujiunga na klabu:
·         Truck suit jozi 1 au 2
·         Bukta jozi 2 na zaidi
·         Viatu vya mazoezi jozi 2
·         Viatu vya mashindano jozi 2
·         Kiasi cha pesa zako binafsi kwa ajili ya kujikimu katika siku za mwanzo
·         Picha passport size 2 kwa ajili ya kumbukumbu za ofisi
·         Shuka na blanketi

  
NB: Kama unakubaliana masharti haya thibitisha kwa kuandika neno NDIO katika nafasi iliyopo………………………..

Saini ya Mchezaji……………………………….
Tarehe……………………………………………..

Saini ya Mzazi/Mlezi………………………….
Tarehe …………………………………………….

Saini ya Mdhamini……………………………..
Tarehe …………………………………………….

Saini ya Afisa michezo Wilaya au Mkoa (muhuri na saini kuthibitisha)……………………….…………………………
Tarehe ……………………………………………..

KARIBU SANA

©
Holili Youth Athletics Club (HYAC)

Saturday, 2 August 2014

ICI C'EST HOLILI YOUTH ATHLETICS CLUB

 MKURUGENZI WA HYAC, DOMICIAN GENANDI

 HEAD QUARTER HYAC, HOLILI

  INNOCENT THOMAS (KATIBU), DOMICIAN GENANDI (CEO), NELSON BRIGHTON (ASSISTANT COACH), TIMOTHY KAMILI(HEAD COACH)



NELSON BRIGHTON (ASSISTANT COACH), TIMOTHY KAMILI(HEAD COACH).