Dickson
ambaye kwa sasa ni moto wa kuotea mbali katika mbio za kilomita 21 (Nusu
Marathon), atawaongoza wenzake Nelson Priva, Alfonce Felix, Saidi Makula,
Lucian Reginald, Catherine Lange, Fadhila Salum, Consolata Samwel, Selina Amos
na Augustino Sulle katika kilomita 21 pamoja na Dotto Ikangaa atakayeshiriki
kilomita 5.
Mkurugenzi
mtendaji wa klabu hiyo, Domician Rwezaura, katika mahojiano maalumu ofisini
kwake alisema kwamba Marwa na wenzake wataondoka Desemba 7 wakiongozana na
viongozi wanne akiwemo kocha wao, Adram Mikumi, Meneja Nelson Mrashani, na
Katibu Innocent pamoja na mwenyewe.
Rwezaura
alisema, mazoezi yanaendelea katika kambi ya mazoezi yaliyoko Tarakea.
Wakati
huohuo, fomu za usajili wa mbio za Uhuru Marathon zimeanza kutolewa siku ya
Jumapili katika ofisi za klabu ya Holili
zilizoko katika jengo la Plaza, mkabala na stendi ndogo ya mabasi ya mjini
Moshi.
No comments:
Post a Comment