Michuano
ya Pune (Poona) International Marathon inatarajiwa kufanyika kesho Jumapili (Desemba Mosi
2013) nchini India, huku Tanzania ikiwakilishwa na wanariadha wawili tu kutoka
katika Klabu ya Holili Youth Athletics.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari mapema leo mchana imesema
wanariadha hao ambao walianza safari yao Novemba 27, mwaka huu ni Oswald
Revelian Kahuruzi ambaye anashiriki mbio hizo kwa mara ya 3 na Pascal Mombo
Sarwat ambaye ni mara yake ya kwanza kushiriki mbio hizo.
Rais
wa Holili Youth Athletics Domician Rwezaura alisema Oswald Kahuruzi atakimbia
mbio hizo katika umbali wa Kilometa 42 wakati Sarwat atakimbia Half Marathon
ambayo ni Kilometa 21.
Blogu
hii ilifanya mahojiano nao majira ya saa 3:35 asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki
kwa saa za India ilikuwa ni saa 6:35 mchana kuhusu mustakabali wao katika mbio
hizo hasa ikizingatiwa wao ni watanzani a pekee wanaoipeperusha bendera.
Kwa
pamoja wanaraidha hao walisema changamoto ni kubwa kutokana na ukweli kwamba
hali ya hewa kwa sasa katika mji huo ni joto hivyo watajitahidi kuipeperusha
bendera.
Hata
hivyo walibainisha kuwa nchi mahiri duniani kwa kutoa wanariadha ambazo ni
Ethiopia na Kenya zimeleta wanariadha wengi ikilinganisha na Tanzania.
Ethiopia
imewaleta wanariadha 100 na Kenya ikiwa na wanariadha 48.
Itakumbukwa
kwamba Pune ni mji ulio karibu kabisa na Jiji Mahiri nchini India la Mumbai.
No comments:
Post a Comment