Mkurugenzi wa Holili Youth
Athletics Club (HYAC), Domician Genandi amehudhuria msiba wa mwandishi habari na
mtangazaji wa michezo Hafidh Henry Lyimo aliyefariki kwa ajali jana usiku,
maeneo ya Mfulie barabara ya Mwika akitokea Rombo katika shughuli zake.
Genandi aliwasili majira ya saa
10 jioni maeneo ya National House (NHC) mjini Moshi ulipo msiba wa mtangazaji
huyo, ambaye alikuwa mdau mkubwa wa HYAC.
Mkurugenzi huyo alisema
amepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha mdau mkubwa ambaye jamii ya Tanzania
haitamsahau kamwe kutokana na mchango wake katika uga wa michezo.
Hata hivyo alito pole kwa
wafiwa kwa tukio hilo la kusikitisha na akuongeza kuwa Mwenyezi Mungu aweze
kuwashikilia wafiwa hao katika kipindi hiki kigumu.
Mwili wa marehemu utazikwa
katika makaburi ya Soweto mjini Moshi Julai 28, mwaka huu.
PREVIOUS
CHAMBER