Wanariadha kutoka visiwani Zanzibar wameng’ara katika urushaji wa kisahani na mkuki katika mbio za taifa mwaka huu, zilizohitimishwa juzi Jijini Dar es Salaam, huku Failuna Abdi wa Arusha na Dickson Marwa wakiwika tena katika mita 10,000 na 5,000.
Tama Jaha (Mjini Magharibi),
Semeni Salmin (Kusini Pemba), Hafsa Ally (Mjini Magharibi) na Khadija Hija
Shukuru (Kusini Pemba) waliibuka washindi katika urushaji wa kisahani (discus),
wakitupa kwa umbali wa mita 31.25, 27.29, 26.48 na 25.77 kwa upande wa
wanawake.
Mkoa wa Dar es Salaam ulishika
nafasi ya nne, ukiwakilishwa na Subira Peter aliyerusha kwa umbali wa mita
26.20
Nafasi ya sita ilishikiliwa na
Theresia Kikanka (Tabora) aliyerusha kisahani kwa umbali wa mita 17.95 na
nafasi ya saba iliwakilishwa na Holo Charles (Mara) akirusha kwa umbali wa mita
16.75
Kwa upande wa urushaji mkuki
(javelin), wanawake Hafsa Ally (Mjini Magharibi) alishika nafasi ya kwanza
akirusha kwa umbali wa mita 37.84, akifuatiwa na MwanaAmina Hassan (Tanga) mita
35.52, Tama Jaha (Mjini Magharibi) mita 35.90
Mkoa wa Pwani ulishika nafasi
ya nne katika urushaji wa mkuki wanawake, ukiwakilishwa na Tumaini James (mita
33.90), mkoa wa Tabora ulishika nafasi ya tano ukiwakilishwa na Theresia
Kikanka (mita 31.20).
Kwa upande wa wanaume, katika
urushaji wa mkuki, mkoa wa Pwani uliongoza na kunyakua nafasi ya kwanza
ukiwakilishwa na Sabas Daniel (mita 54.76).
Nafasi ya pili ilishikwa na
Daniel Mollel (Arusha) akirusha mkuki kwa umbali wa mita 53.50, Gilia Shagembe
kutoka Tabora alishika nafasi ya tatu kwa umbali wa mita 51.02
Mkoa wa Dar es Salaam ulishika
nafasi ya nne ukiwakilishwa na Charles Ibrahim aliyerusha mkuki kwa umbali wa
mita 50.47 huku Said Thomas wa Arusha akimaliza watano kwa umbali wa mita 49.81
Failuna Abdi na Dickson Marwa
baada ya kung’ara katika siku ya kwanza wakifanya vizuri katika mita 5,000 na
10,000; jana wameibuka washindi katika siku ya mwisho ya mbio hizo za taifa.
Mwanariadha Failuna Abdi
aliuwakilisha vilivyo mkoa wa Arusha akishika nafasi ya kwanza, baada ya
kukimbia kwa muda wa dakika 33:32.80 mita 5,000.
Nafasi ya pili ilishikwa na
Catherine Range (Arusha) akifukuza upepo kwa muda wa dakika 34:00.15 akifuatiwa
na Magdalene Chrispine (Kagera) alikimbia kwa muda wa 36:17.53
Mkoa wa Kagera ulimaliza tena
katika nafasi za nne na tano kwa tiketi ya wanariadha wake Furaha Sabaya (dk.
39:15.24) na Irene Chima (dk. 40:78.16).
Dickson Marwa aliwanyanyua mashabiki
wa mkoa wa Mara, aking’ara tena katika mbio za mita 5,000 akitumia muda wa dk.
13:38.48 na kuwapiku Fabian Nelson (Kilimanjaro), Joseph Teofil (Arusha),
Gabriel Gerald (Kilimanjaro) waliokimbia kwa muda wa dk. 13:39.58, 13:40.29 na
13:45.26
Mkoa wa Kagera katika mita 5,000
wanaume ulishika nafasi ya tano ukiwakilishwa na Paul Goti aliyekimbia kwa muda
wa dakika 13:59.06 akimpita Josephat Joshua (Kilimanjaro), Shamba Kitime
(Arusha), Joseph Sule (Arusha) wakikimbia kwa muda wa dk. 13:59.55, 14:02.16,
na 14:05.04
Hata hivyo katika siku ya
mwisho kulijitokeza dosari nyingine ambayo iliwakuta baadhi ya waamuzi
walipojikuta wakishangilia wakati wanariadha wakichukuana katika mbio za
uwanjani hapo hivyo kusababisha uchukuaji wa rekodi kuwa mgumu, nusura ngumi
zichapwe baina yao na wanariadha.
Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha
Tanzania (RT), Suleiman Nyambui alipohojiwa kuhusu sakata hilo alijitetea
kwamba kila kitu waliachiwa kamati ya maandalizi wakati yeye alipokuwa nchini
New Zealand.
Aidha Nyambui aliongeza kusema
baada ya dosari lukuki kujitokeza katika mbio hizo za taifa mwaka huu, watakaa
kitako kufanya upembuzi yakinifu likiwemo suala la uzoefu alioupata nje ya nchi
kwa miezi takribani miwili aliyokaa.
No comments:
Post a Comment