Tasnia
ya Habari na wanamichezo mkoani Kilimanjaro imepata pigo kufuatia kifo cha
ghafla cha Mtangazaji wa kituo cha redio Moshi FM Hafidh Henry Lyimo “Kipese” .
Kipese
amefariki dunia usiku wa jana majira ya saa 2 akiwa njiani akitokea Rombo
katika eneo la makutano ya barabara ya Mwika baada ya pikipiki aliyokuwa
akitumia kugongana na pikipiki nyingine.
Taarifa
za awali zinasema Marehemu Kipese alikuwa akitokea wilayani Rombo ambako
amekuwa akifanya shughuli zake na kwamba wakati anarejea ndipo mauti yakamfika
baada ya kuumia vibaya katika ajali hiyo.
Kipese
alikuwa katika pikipiki aina ya Toyo yenye namba za usajili T 115 CAU
Katika hatua ya kwanza mwili wa marehemu ulihifadhiwa katika hospitali ya Kilema wilayani Moshi vijijini kungojea taratibu nyingine toka kwa ndugu zake ambapo Julai 27 mwaka huu mwili huo ulihamishiwa katika Hospitali ya KCMC mjini Moshi.
Tayari
makundi mbalimbali ambayo marehemu amekuwa karibu nayo kwa shughuli za kikazi
yametoa taarifa za masikitiko kufuatia kifo cha Kipese.
Makundi
hayo ni Wanahabari mkoani Kilimanjaro, Vyama vya Michezo mkoani humo kikiwemo
KRFA, na wadau wa michezo mkoani
Kilimanjaro ambako licha ya kwamba Marehemu Kipese alikuwa mtangazaji wa
kipindi cha Michezo katika redio aliyokuwa akifanyia kazi pia alikuwa mwamuzi
wa mchezo wa soka.
Safari ya mwisho ya Marehemu
Hafidh Lyimo itakuwa kesho (Julai 28, mwaka huu) katika makaburi ya Soweto mjini Moshi
PREVIOUS CHAMBER
CHANZO:
JAIZMELALEO
No comments:
Post a Comment