Mbio za Uhuru Marathon 2014 zimegeuka shubiri
kwa mwanariadha mkongwe, Fabian Joseph baada ya kukumbana na mkasa wa kung'atwa
kidole kama ilivyokuwa kwa beki wa Italia, Giorgio Cheillini ambaye aling'atwa
bega na mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez kwenye fainali za Kombe la Dunia
nchini Brazil.
Katika mbio hizo zilizohitimishwa jana katika
viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam, Fabian alikumbana na mkasa huo
baada ya kumaliza mbio, na ndipo wakaanza kuzozana na mpinzani wake kutoka
Mbulu, Deo Lazaro aliyechukua hatua ya kumng'ata kidole.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mara baada ya tukio hilo, mratibu wa mbio hizo, Innocent Meleck, alisema kitendo kilichofanywa na Lazaro si cha kiungwana na kwamba hata kama walikuwa na ugomvi hapo kabla hakupaswa kufanya hivyo.
Alisema kutokana na kufanya hivyo, Lazaro alipelekwa Polisi, na Fabian aliyefanikiwa kumaliza mbio hizo akiwa wa kwanza alipelekwa hospitali ya Mwananyamala na kupata matibabu na baadaye kuruhusiwa.

Hata hivyo, kocha wa wanariadha hao ambaye
alikataa kutaja jina lake, alisema Lazaro alimng'ata Fabian kutokana na
kuchanganyikiwa na hali ya hewa ya joto ya jijini Dar es Salaam.
"Deo hawezi kumng'ata Fabian hivi hivi, alichanganyikiwa na hali ya joto na kuanza kupigana na mwenzake na hivyo kumng'ata kidole. Kwa sasa (jana saa 10:00 alasiri) wote wapo Hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya kuangaliwa afya zao," alisema kocha huyo.
Katika fainali hizo kwa upande wa mbio za Marathon, Fabian ameshika nafasi ya kwanza baada ya kutumia muda 1:05:09, huku nafasi ya pili ikienda kwa Alphonce Felix aliyetumia saa1:05:15, nafasi ya tatu imekwenda kwa Elia Dandi ambaye alitumia 1:05:22, wakati ya nne imechukuliwa na Ezekiel Ngimba aliyetumia 1:06:25.

Katika mbio za kilomita tano wanawake, Marrium
Salum alishika nafasi ya kwanza, akifuatiwa na Grace Jackson huku ya tatu
ikienda kwa Adelina Trasims, wakati wanaume ni Muhamed Nyambui nafasi ya
kwanza, ya pili ikienda kwa Peter Sinde na ya tatu ikiwa halali ya Hafidhi
Hafaa.
No comments:
Post a Comment