HYAC
Tuesday, 14 October 2014
Saturday, 11 October 2014
Thursday, 2 October 2014
HOLILI YAJIPANGA ROTARY MARATHON 2014
Wanariadha kutoka katika klabu
ya riadha ya Holili Youth (HYAC) wamejinasibu kufanya vizuri katika mbio za
Rotary Marathon zinazotarajiwa kufanyika Oktoba 14 mwaka huu, Jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza Mkurugenzi wa HYAC,
Domician Genandi alisema wanariadha wake wana ari na shauku ya kufanya vizuri
baada ya kujinoa kwa muda mrefu katika kambi waliyojichimbia katika kijiji cha
Holili, wilayani Rombo.
“Mazoezi ya kutosha wamefanya
chini ya kocha Timothy Kamili, tunajiamini kuelekea mbio hizo ambapo tuna ari
ya kuibakisha rekodi safi ya mwaka uliopita klabuni hapo ambapo Alphonce Felix
alitwaa nafasi ya kwanza” alisema Domician.
Genandi aliongeza kusema mbio hizo ambazo zitakuwa za kilomita 21
(half Marathon) zitasaidia kukuza wanariadha wake kuelekea mbio ndefu (full
marathon) kutokana na ukweli kwamba Tanzania bado haijapata wakimbiaji wazuri
wa mbio ndefu.
Pia Mkurugenzi huyo aliwataja
wanariadha wanne ambao watajitupa katika mbio hizo kusaka taji la ushindi mwaka
huu kuwa ni Pascal Mombo, Elibariki Buko, Lameck Misiwa na mwanadada Furaha
Sambeke.
Hata hivyo aliweka bayana
kuhusu wanariadha wengine wanaonolewa katika klabu hiyo pekee hapa nchini kuwa
wanaendelea kuwapa mazoezi ya nguvu kwa
ajili ya mbio zijazo.
Aidha Domician aliwataka wadau
wa mchezo wa riadha nchini kujitokeza kuwekeza kwa wanariadha ili kuwepo na
ushindani ambao utakuwa chachu ya mafanikio pindi michuano ya kimataifa
inapokaribia.
“Tanzania ina wanariadha wengi
wazuri, lakini changamoto ipo katika uwekezaji haupo kwa wanariadha hao hali
inayodumuza vipaji hivyo, kwani mwanariadha akifanya mazoezi peke yake bila
makocha na waangalizi hawezi kufanya inavyostahili” alisema Domician.
Saturday, 27 September 2014
PROSECIUS PROSPER APATA NAFUU
Mwanariadha Procesius Prosper wa HYAC amepata nafuu baada ya kuzimia asubuhi ya Septemba 25 mwaka huu kabla hajaenda
mazoezini.
Prosecius hukimbia mbio fupi.
Monday, 15 September 2014
CEO-HYAC AFIWA NA DADA YAKE
CEO-HYAC,
Domician Genandi
Uongozi
na wachezaji wa Klabu ya Holili Youth Athletics (HYAC) unatoa pole kwa Mkurugenzi
Mkuu Domician Genandi kwa kuondokewa na dada yake kipenzi.
Mazishi
yamepangwa kufanyika mkoani Kagera na sasa ndugu jamaa na marafiki wapo mkoani
Kagera kuhudhuria msiba huo.
Mwenyezi
Mungu awafariji wafiwa
AMEN.
UTAWALA
Friday, 5 September 2014
KONA YA PRO, JULAI 2014: USAIN BOLT ATISHA JUMUIYA YA MADOLA
BIOGRAPHY
CHAMBER
Katika
kipengele hiki leo tutamwangazia Mwanariadha mwenye kasi duniani kwa sasa Usain
Bolt ambaye ni shabiki mkubwa wa klabu ya Manchester United ya nchini England.
Usain
Bolt St Leo alizaliwa Agosti 21, 1986, Trelawny, nchini Jamaika kwa sasa ni
mwanariadha aliyeshinda medali tatu za dhahabu katika mashindano ya Olimpiki.
Anashikilia rekodi ya dunia ya sasa katika wote 100 na 200 dash mita na alama
ya 9:58 na sekunde 19:19 mtiririko huo. Got alama hizi katika XII ya Mabingwa
wa Dunia uliofanyika katika Berlin. Hasa, Bolt imeweza kuvunja rekodi kwa dash
mita 100 Agosti 16, 2009 [2] na mita 200 kwa siku nne baadaye, tarehe 20 Agosti
2009.
Usain
Bolt ana rekodi ya dunia katika dash mita 4x100 kwa njia ya muda 36.84 sekunde,
mafanikio katika michezo ya Olimpiki Summer mwaka 2012 timu ya Nesta Carter,
Michael Frater, Yohan Blake na Usain Bolt [4] zaidi ya rekodi ya zamani ya sekunde
37.04 pia uliofanyika katika Jamaica. Na ushindi mshindi wa Olimpiki yake ya
sita ya dhahabu, na tonra kushinda kutetemeshwa ya Beijing kufikiwa 100, 200 na
4x100.
Mwaka
2008 na 2009 alitambuliwa na IAAF kuwa mwanariadha wa mwaka wa shirikisho hilo. Pia mwaka 2009 serikali
ya nchi yake alitunukwa tuzo ya Amri ya Jamaica, hivyo kuwa mtu mdogo kupokea
tuzo hiyo.
Bolt
ameweka rekodi nchini mwake kwa kuwa m-Jamaika wa kwanza kushinda mbio za mita
100 na mita 200 katika Michezo ya Olimpiki mbili mfululizo.
Michuano na matokeo
- 2002 Dunia Vijana ya Mabingwa 2002 Kingston, Jamaica 1 mita 200 20.61 s
- 2002 Dunia Vijana ya Mabingwa 2002 Kingston, Jamaica 2 4x100m relay 39.15 s
- 2002 Dunia Vijana ya Mabingwa 2002 Kingston, Jamaica 2 4x400m relay 03:04:06 s
- 2003 Dunia ya Vijana michuano ya 2003 Shinyanga, Canada 1 200m s 20:40
- 2007 Mabingwa wa Dunia 2007 Osaka, Japan 200 m 19.91 s 2
- 2007 Mabingwa wa Dunia 2007 Osaka, Japan 2 4x100m relay 37.89 s
- 2008 Michezo ya Olimpiki ya Beijing mwaka 2008, China 1 mita 100 9.69 s
- 2008 Beijing Michezo ya Olimpiki, China ni 1 ya mita 200 AU 19:30
- 2008 Michezo ya Olimpiki ya Beijing mwaka 2008, China 1 4x100m relay 37.10 s
- 2009 Mabingwa wa Dunia 2009 Berlin, Ujerumani 1 100m WR ni 09:58
- 2009 Mabingwa wa Dunia 2009 Berlin, Ujerumani 1 200m 19.19 s WR
- 2009 Mabingwa wa Dunia 2009 Berlin, Ujerumani 1 4x100m relay 37.31 s
- 2011 Mabingwa wa Dunia 2011 Daegu, Korea 1 200 m s 19:40
- 2011 Mabingwa wa Dunia 2011 Daegu Korea ya Kusini 1 4x100m relay 37.04 s
- 2012 Michezo ya Olimpiki 2012 London, Uingereza 1 mita 100 9.63 s AU
- 2012 Michezo ya Olimpiki 2012 London, Uingereza 1 200 m s 19:32
- 2012 Michezo ya Olimpiki 2012 London, Uingereza 1 4x100 relay 36.84 s WR
Prepared
by:
Jabir
Johnson
Blogger
& Photo Journalist
+255-(0)-768
096 793
Subscribe to:
Posts (Atom)



