HYAC

Attack with Style, Defend with Heart

Friday, 27 December 2013

HOLILI YOUTH ATHLETICS CLUB YAALIKWA ZANZIBAR JANUARI 12



HOLILI

Klabu pekee ya Riadha nchini Tanzania, Holili Youth Athletics Club (HYAC) ya Wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro inatarajiwa kushiriki Mashindano ya Riadha ya Sherehe za Mapinduzi kutimiza miaka 50 ya uhuru wa Visiwa hivyo.
MIONGONI MWA WANARIADHA WA HYAC WAKIWA KATIKA KARATU SPORTS FESTIVAL 2013
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Menejimenti ya Klabu hiyo ilisema Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Taifa Suleiman Ame Hamis aliwaandikia barua ya mwaliko yenye Kumbukumbu Na. CRT/Z/VOL II/IMU/1147 ya kuwataka kuhudhuria sherehe hizo.

Taarifa ya Menejimenti hiyo iliongeza kusema Chama cha Riadha Zanzibar (ZAAA) kimetaka kuandaa timu ya wanariadha wataokwenda kushiriki mbio hizo.

Hata hivyo ZAAA imewataka kujigharimia wenyewe kuelekea kufanikisha mbio hizo  maalum kabisa kwa ajili ya miaka 50 ya uhuru wa Zanzibar.

Akizungumza, Meneja wa Klabu Nelson Mrashani aliongeza kusema timu yake ipo tayari kutokana na ukweli kwamba wachezaji wake wapo kwenye Kambi Tarakea mpakani mwa Tanzania na Kenya hivyo ni suala la kuchagua idadi ya watakaokwenda kuwakilisha.

Hata hivyo alitanabaisha kuwa hawataweza kupeleka wanariadha wengi kutokana na ufinyu wa bajeti ya klabu hiyo hasa ikizingatiwa kwamba mpaka sasa haijapata wafadhili wowote kwa ajili ya kuwasaidia kufikia malengo.

Mkurugenzi wa Klabu hiyo Domician Genandi aliwataka wadau kote nchini kujitokeza kwa wingi kuunga mkono juhudi za kuinua riadha Tanzania kwa kutoa michango yao ya hali na mali katika klabu yake.

Aidha alitanabaisha kuwa HYAC imejipanga kuifikia mikoa yote nchini kwa ajili ya kuvumbua vipaji na hata safari ya Zanzibar ni muhimu kwao kwani vipaji vitakavyoonekana havitaachwa kamwe.

IRENE ASIA CHIMA

REKODI ZA WANARIADHA WA HOLILI YOUTH ATHLETICS CLUB (HYAC)
 
Klabu hii imejizatiti katika kufikia malengo ikiwemo kutunza kumbukumbu za wachezaji wake, huku ikijua wazi kwamba kumbukumbu hizi husaidia kuboresha maendeleo ya mchezaji mwenyewe na jamii kwa ujumla.
 
REKODI HIZI NI KUANZIA DESEMBA 2013 HADI SASA

IRENE ASIA CHIMA
 
IRENE ASIA KATIKA KARATU SPORTS FESTIVAL 2013
Tarehe ya Kuzaliwa (DoB)
Mei 25, 1992
Mahali Alipozaliwa (PoB)
Makiungu, Singida

USHIRIKI KATIKA MBIO MBALIMBALI

Tarehe
Aina ya Mbio
Muda Aliotumia
 Mahali Ilipofanyika
Des. 21, 2013
Karatu Sports Festival 2013

5 km
Dakika 22:01.84
Karatu Town
 

NEEMA MATHIAS MSWADI



REKODI ZA WANARIADHA WA HOLILI YOUTH ATHLETICS CLUB (HYAC)
Klabu hii imejizatiti katika kufikia malengo ikiwemo kutunza kumbukumbu za wachezaji wake, huku ikijua wazi kwamba kumbukumbu hizi husaidia kuboresha maendeleo ya mchezaji mwenyewe na jamii kwa ujumla.
 
REKODI HIZI NI KUANZIA DESEMBA 2013 HADI SASA
NEEMA MATHIAS MSWADI
 

NEEMA MATHIAS KATIKA KARATU SPORTS FESTIVAL 2013
Tarehe ya Kuzaliwa (DoB)
Machi 10, 1999
Mahali Alipozaliwa (PoB)
Mtamaa, Singida

USHIRIKI KATIKA MBIO MBALIMBALI

Tarehe
Aina ya Mbio
Muda Aliotumia
 Mahali Ilipofanyika
Des. 21, 2013
Karatu Sports Festival 2013

5 km
Dakika 20:42.23
Karatu Town
Des. 4, 2013
Serengeti Marathon

21 km
 Saa 1:30.23
Mara-Mwanza