HOLILI
Klabu
pekee ya Riadha nchini Tanzania, Holili Youth Athletics Club (HYAC) ya Wilayani
Rombo Mkoani Kilimanjaro inatarajiwa kushiriki Mashindano ya Riadha ya Sherehe
za Mapinduzi kutimiza miaka 50 ya uhuru wa Visiwa hivyo.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Menejimenti ya Klabu hiyo ilisema Katibu Mkuu
wa Chama cha Riadha Taifa Suleiman Ame Hamis aliwaandikia barua ya mwaliko
yenye Kumbukumbu Na. CRT/Z/VOL II/IMU/1147 ya kuwataka kuhudhuria sherehe hizo.
Taarifa
ya Menejimenti hiyo iliongeza kusema Chama cha Riadha Zanzibar (ZAAA) kimetaka
kuandaa timu ya wanariadha wataokwenda kushiriki mbio hizo.
Hata
hivyo ZAAA imewataka kujigharimia wenyewe kuelekea kufanikisha mbio hizo maalum kabisa kwa ajili ya miaka 50 ya uhuru
wa Zanzibar.
Akizungumza,
Meneja wa Klabu Nelson Mrashani aliongeza kusema timu yake ipo tayari kutokana
na ukweli kwamba wachezaji wake wapo kwenye Kambi Tarakea mpakani mwa Tanzania
na Kenya hivyo ni suala la kuchagua idadi ya watakaokwenda kuwakilisha.
Hata
hivyo alitanabaisha kuwa hawataweza kupeleka wanariadha wengi kutokana na
ufinyu wa bajeti ya klabu hiyo hasa ikizingatiwa kwamba mpaka sasa haijapata
wafadhili wowote kwa ajili ya kuwasaidia kufikia malengo.
Mkurugenzi
wa Klabu hiyo Domician Genandi aliwataka wadau kote nchini kujitokeza kwa wingi
kuunga mkono juhudi za kuinua riadha Tanzania kwa kutoa michango yao ya hali na
mali katika klabu yake.
Aidha
alitanabaisha kuwa HYAC imejipanga kuifikia mikoa yote nchini kwa ajili ya
kuvumbua vipaji na hata safari ya Zanzibar ni muhimu kwao kwani vipaji
vitakavyoonekana havitaachwa kamwe.
No comments:
Post a Comment