Serengeti Marathon zilianza mapema ya Desemba 4 mwaka huu
katikati ya mbuga za Serengeti wilayani Bunda mkoani Mara kwa kufunguliwa na
Mkuu wa Wilaya hiyo Joshua Milumbe.
WANARIADHA
KUTOKA BUSEGA, JOHN KABUTI, ALI JUMA NA ISSA JUMA WAKIWA KATIKA MBUGA ZA
SERENGETI TAYARI KUANZA KUFUKUZA UPEPO.
|
Ambapo katika ufunguzi huo wanariadha zaidi ya 100
walihudhuria na kushuhudia mbio hizo zikianza ndani kidogo ya geti la Ndabaka yapata
kilometa 3.5 kutoka barabara iendayo Musoma-Mwanza.
Muasisi wa Mbio hizo Dk. Titus Kamani alishiriki mbio hzio
licha ya kwamba alikimbia kilometa 5 kwa uzinduzi na kushika nambari moja huku
akishuhudiwa na washiriki wengine.
William Mwakilema, Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Serengeti
ambayo imo katika maajabu makubwa hapa ulimwenguni alisema mbio hizo zinazidi
kutia hamasa na kuendeleza vita dhidi ya wale wanaowinda wanyamapori pasipo
kufuata taratibu na kanuni za wanayamapori.
Wanariadha watoto kutoka familia moja Issa Juma (14)
anayesoma darasa la 5 na Ali Juma (12) anayesoma darasa la 4 mwingine wa nyumba
ya jirani yao John Kabuti (13) anayesoma darasa la 3 walikimbia mbia za
kilometa 5.
ULINZI ULIKUWEPO KATIKA MBIO HIZO HASA IKIZINGATIWA
WANYAMAPORIKAMA SAWALA, PUNDAMILIA, KONGONI NA WENGINEO WALIKUWA KARIBU SANA.
|
WANARIADHA KUTOKA NDANI NA NJE YA NCHI WALISHIRIKI SERENGETI
MARATHON
|
DK. TITUS KAMANI MUASISI WA SERENGETI MARATHON AKIZUNGUMZA
JAMBO KATIKA UFUNGUZI WA MBIO HIZO.
|
MHIFADHI MKUU WA HIFADHI YA SERENGETI, WILLIAM MWAKILEMA
AKIZUNGUMZA JAMBO PEMBENI NI JOSHUA MILUMBE MKUU WA WILAYA YA BUNDA.
|
WANARIADHA WA FULL MARATHON (KILOMETA 42) WALIANZA KUTIMUA
MBIO HIZO
|
KUTOKA KUSHOTO, DK. TITUS KAMANI, JOSHUA MILUMBE NA
WANARIADHA WATOTO TISHIO LA KESHO KABLA YA KUANZA KILOMETA 5
|
MTAYARISHAJI: JOHNSON JABIR
ITAENDELEA…
No comments:
Post a Comment