Wanariadha
6 wa Holili Youth Athletics Club wanatarajia kukimbia mbio za Karatu Ten – K zitakazofanyika
Jumamaosi ya Desemba 21 mwaka huu.
NEEMA
MATHIAS
|
Msemaji
wa Holili Youth Athletics Club Johnson Jabir amewaambia waandishi habari kuwa
wanawake watakuwa wawili ambao watakimbia kilometa 5.
Amewataja
wanariadha hao wa kike kuwa ni Neema Mathias ambaye ana rekodi ya kukimbia mbio
za Kilometa 21 za Serengeti Marathon na kushika nafasi ya 3 nyuma ya Furaha
Sambeke na Mary Naali; na mwanamke mwingine ni Irene Asia.
Msemaji
huo ameongeza kusema wanaume watakuwa 4 ambao ni Mapacha Francis Makombe na
Richard Makombe, Wambura Lameck ambaye anashikilia rekodi ya pekee katika mbio
za Uhuru Marathon mwaka huu na Nelson Priva.
Hata
hivyo amesema Timu hiyo itaondoka kambini Tarakea Wilayani Rombo kesho mchana (Desemba
20, 2013) na kuwasili Kaaratu mkoani Arusha siku hiyo hiyo jioni ambapo
itaongoza na Uongozi mzima wa timu hiyo pekee nchini Tanzania.
Viongozi
watakaombatana na Timu hiyo ni Mkurugenzi Domician Genandi, Meneja wa Timu
Nelson Mrashani na Katibu wa Timu Innocent Mushi.
Itakumbukwa
kwamba Ushiriki wa Holili Youth Athletics Club ni muhimu mno hasa ikizingatiwa
kuwa ina malengo ya kushiriki kila mbio kwa ajili ya kusaka vipaji na kuviinua.
No comments:
Post a Comment