*Wajigamba
kufanya vizuri
*Dickson
Marwa, Sambu Andrew wanatarajiwa kuwemo
*
Flora Yuda aliibuka mshindi wa 4 Serengeti Marathon anatarajiwa kushiriki Half
Marthon
Uhuru Marathon inatarajiwa
kuanza kutimua mbio zake hapo kesho jumapili ya Desemba 8 mwaka huu ikiwa ni
siku moja kabla ya maadhimisho ya miaka 52 ya uhuru wa Tanzania Bara.
Wakati hayo yakijiri Holili
Youth Athletics Club (HYAC) ikiwa ni kalbu pekee nchini Tanzania inayojihusisha
na riadha imethibitisha kuwasili kwa timu ya wakimbiza upepo akali ya 12 jioni
ya leo Jijini Dar es Salaam.
Msemaji wa Klabu hiyo Johnson
Jabir alisema timu ya wafukuza upepeo kutoka klabu hapo mkoani Kilimanajro
imewasili majira ya saa 11 jioni leo Jumamosi ikitokea mkoani humo.
Hata hivyo HYAC imejigamba
kufanya vizuri ikilinganishwa na Serengeti Marathon kutokana na ukweli kwamba
hali ya hewa Jijini Dar es Salaam ni nzuri na wachezaji wengi wa klabu hiyo
wamezoea kukimbia katika barabara za lami hivyo itakuwa kazi rahisi kwao
kufanya vizuri.
Mbio hizo zinatarajiwa kuanza
mnamo saa 12:30 katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam.
Itakumbukwa kwamba Desemba 4
mwaka huu wanariadha 4 kutoka HYAC walishiriki Serengeti Marathon iliyofanyika
mkoani Mwanza ikianzia mkoani Mara katika Wilaya ya Bunda.
No comments:
Post a Comment