W
|
anariadha Furaha Sambeke na Neema
Mathias , wa Holili Youth Athletics Club wameiwakilisha vyema kabla hiyo katika
mbio za Pili za Serengeti Marathon mwaka 2013 baada ya kushika nafasi za pili
na tatu kwa upande wa Wanawake.
NEEMA
MATHIAS AKIPOKEA MKONO WA PONGEZI NA MHESHIMIWA TITUS KAMANI MBUNGE WA BUSEGA
|
Wanariadha hao wa kike
walikimbia mbio za kilometa 21 (Half Marathon) wakiachwa na mkongwe Mary Naali
wa mkoani Arusha kwa dakika 10.
Mbio hizo ambazo zilianza
mapema majira ya saa moja asubuhi ya Desemba 4, mwaka huu katikati ya Hifadhi
ya Wanyama ya Serengeti karibu na geti la Ndabaka wilayani Bunda mkoani Mara kwa
wafukuza upepo kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Mary Naali alimaliza mbio hiyo
katika kijiji cha Lukungu, kilichopo Lamadi wilayani Busega Mkoani Mwanza kwa
kutumia muda wa 1:16:45.
Furaha Sambeke alimaliza mbio
hizo kwa muda wa 1:26:24 wakati Neema Mathias alihitimisha safari yake kwa muda
wa 1:30:23.
Washindi wengine katika mbio
hizo walikuwa Magret Gilbert kutoka Urambo Tabora aliyekimbia kwa
muda wa 1:35:02 akifuatiwa na Anna
Kabote alifunga nafasi tano bora kwa muda wa 1:35:54
IN
BRIEF:
SERENGETI MARATHON 2013
Kilometa 21
|
NAFASI
|
JINA
|
MUDA
|
ANAKOTOKA
|
1.
|
Mary
Naali
|
1:16:45
|
Arumeru
- Arusha
|
2.
|
Furaha
Sambeke
|
1:26:24
|
Holili
Youth Athletics Club
|
3.
|
Neema
Mathias
|
1:30:23
|
Holili
Youth Athletics Club
|
4.
|
Magreth
Gilbert
|
1:35:02
|
Urambo
- Tabora
|
5.
|
Anna
Kabote
|
1:35:54
|
Busega
-Simiyu
|
·
PICHA ZAIDI
KUHUSU SERENGETI MARATHON ZITAKUJIA BAADAYE
No comments:
Post a Comment