Kila
mwaka unapofika mwezi Desemba, watu mbalimbali ulimwenguni pote, kila mmoja kwa
tamaduni ya eneo analoishi huwepo shamrashamra, vifijo na nderemo.
JOHNSON JABIR
|
Nchini
Tanzania watu wa jamaa, makabila mbalimbali huanza purukushani za kumaliza
mwaka, mojawapo ikiwa ni maandalizi ya sherehe za Kuzaliwa kwa Yesu (Krismas)
na Mwaka Mpya.
Waumini
wa dini ya Kikristo huwa na shamrashamra zaidi ya wengine kutokana na ukweli
kwamba sikukuu ya Krismas hupendwa sana kutokana na wao kumjua zaidi Kristo
Yesu.
Desemba
2013, niliona vema nitue katika mji mdogo ulio maarufu sana nchini Tanzania, wa
Holili. Huenda ni maarufu kutokana na sababu lukuki lakini moja kati hizo ni
uwepo wa kituo cha mpaka kati ya Tanzania na Kenya.
Sio
mara yangu ya kwanza kufika Holili, kwa mara ya kwanza ilikuwa Desemba 2012
nilipongia mkoani Kilimanjaro nikiwa na mwezi mmoja tulifika na rafiki yangu
aliyefahamika kwa jina la Edward Haule.
Nilipofika
hapo nilipokewa na familia moja maarufu sana mjini humo ya jamaa mmoja anafahamika
kama Domician Genandi Rwezaura.
Ukifika
hapo, ukiuliza “Domi” hakuna asiyemjua, mtoto hata mkubwa watakuambia na
kukueleza anapoishi.
Nilistaajabu
sana kukutana watu kadha wa kadha wakimfahamu huyu anafahamika kwa jina la “Domi”.
Nikaamua
kuwauliza nini hasa, wakaniambia kwamba Domi ni mfanyabiashara, licha ya kazi
yake hiyo lakini kubwa zaidi ni mcheshi sana kwa watu wa eneo hilo tangu
wameanza kufahamu kwani kuna wafanyabiashara wengi lakini iweje huyo pekee?
Nikafurahi
sana kusikia maneno hayo ya faraja kutoka kwa watu wa eneo hilo.
Desemba
23, 2013 alinipokea na kunipeleka katika eneo
mojawapo la biashara zake linalojulikana kwa jina la “KWETU PAZURI”.
Nikastaajabu
kwa mara nyingine kwanini panaitwa
“KWETU PAZURI” hasa nikikumbukwa waimbaji
kutoka nchini Rwanda wa Christ Ambassadors waliowika na Albamu yao ya “KWETU
PAZURI” miaka 2010.
Nikaambiwa
hapo wengi wanapapenda kutokana na huduma nzuri wanazopata hapo ukilinganisha
na mahali pengine mjini humo. Utakutana na vinywaji, vyakula vizuri na hata
ukumbi wa kutazama mechi mbalimbali za soka kwa wale wapenda soka na filamu.
Nikala
chakula kizuri, mimi ni mpenzi mno wa Wali Kuku na Soda nikafurahi kweli kwani
kilikuwa kizuri hadi nikahisi hakuna haja ya kuondoka mapema ulimwenguni.
Baada
ya hapo hali ya mambo ikaanza kuwa nzuri lakini Domi akanipa taarifa kwamba
Desemba 26, 2013 angekuwa sherehe ya
binti yake Winny alikuwa akipata Komunyo katika Kanisa la Katoliki Sinai-Holili.
Krismas
iliwadia waliamka na kwenda kanisani hapo hapo Holili, mimi siku hiyo sikwenda
kabisa nilibaki nalala tu kutokana na kazi nzito nilizokuwa nikikamilisha siku
ya nyuma.
Jioni
yake tuliwajibika kwa miongoni mwa majirani aliyefahamika kwa jina la Kessy
katika kusheherekea siku hiyo , hakika
ilikuwa ya kupendeza kuliko kawaida, tulikula, tukanywa vile tunavyovipenda
hatimaye giza likaanza kulinyemelea anga ndipo nilipoondoka na kwenda kulala
sehemu niliyofikia ya “Afrika Sana”.
WINFRIDA
“WINNY” RWEZAURA
|
Ilikuwa
ni Alhamis ya Desemba 26, ndugu, jamaa na marafiki walijumuika pamoja katika
sherehe hizo kwa familia ya Domi.
Itakumbukwa
kwamba Domi ni mzaliwa wa Kijiji cha Maziba mkoani Kagera (zamani Ziwa
Magharibi) hivyo sikushangaa nilipokuwa nikisikia lafudhi za kutoka huko napo
pia nilihisi kuwa sisi ni watanzania kweli kweli.
Nasema
hivyo kwasababu, hakuna aliyeniuliza mimi ni kutoka kabila gani na mkoa gani
nami nikaonekana miongoni mwa familia ya jamaa huyo ambaye hakika ni mcheshi.
Utafurahi ukikaa naye!!
Winfrida
“Winny” Rwezaura ni miongoni mwa watoto wa Domi wengine ni Karen “Kukugonza” na
Genandi “Rwechungura” alizaliwa Agosti 17, 2003.
No comments:
Post a Comment