labu
ya Holili Youth Athletics Club (HYAC) ya mjini Holili, mkoani Kilimanjaro,
imejitosa kudhamini mbio za Sokoine Mini Marathon zinazotarajiwa kufanyika
Aprili 12, mwaka huu katika Kijiji cha Monduli Juu, Wilaya ya Monduli, mkoani
Arusha.
|
Domician Genandi,
Managing Director
(HYAC).
|
Katika
udhamini huo, HYAC imetoa sh milioni moja zitakazotumika kuchapisha namba
(Bibs), 1,000 za utambulisho za wanariadha.
Akizungumza
na vyombo vya habari Mkurugenzi
wa HYAC, Domician Genandi, alisema kilichomsukuma kufanya hivyo ni moyo wa
uanamichezo na kuongeza kuwa, kwa mwaka huu wamedhamiria kuongeza nguvu zote
kuinua mchezo wa Riadha nchini.
“Nimeamua
kusaidia nikiwa kama mdau, sababu lengo letu ni kuendeleza michezo Tanzania,
sisi wadau tunatakiwa tuwe na mtazamo wa ushindi kama taifa na si ushindi wa
klabu zetu binafsi tu, au wanariadha wetu tu, HYAC tunatambua jitihada binafsi
zinazofanywa na waandaaji kumuenzi hayati Sokoine,” alisema Genandi.
Aidha,
Genandi alisema kwa mwaka huu klabu yake inatarajiwa kushirikisha wanariadha
wengi zaidi, ambako lengo lake ni kuhakikisha anaendeleza rekodi ya mwaka jana.
Hata
hivyo Mkurugenzi huyo alitaka Sokoine Mini Marathon ifanyike siku moja kabla ya
tukio ili wanariadha nao wapate muda wa kuhudhuria maadhimisho ya mkongwe huyo
kisiasa hapa nchini hasa ikizingatiwa kwamba maadhimisho hubeba vitu vingi.
Pia
Domician alitanabaisha siku moja kabla inainua uchumi wa eneo husika hivyo siku
zinapokuwa chache hufanya uchumi kukua taratibu kutokana na ukweli kwamba maadhimisho
hayo hukusanya washiriki wengi kila mwaka.
Kwa
upande wake, Mratibu wa mbio hizo, Wilhelm Gidabuday alisema kwa udhamini huo
HYAC inakuwa klabu ya kwanza ya riadha hapa nchini kudhamini mashindano
yanayoandaliwa na wadau wengine wa riadha na kuongeza kuwa, katika hilo
wameonesha kweli kwamba wana nia nzuri ya kuendeleza michezo hapa nchini hasa
riadha.