NELSON
MRASHANI
|
Nelson Brighton Mrashan ni
miongoni mwa makocha wa mchezo wa Riadha waliohitimu mafunzo ya ukocha ngazi ya
pili ya cheti.
Nelson Mrashan alihitimu
mafunzo hayo Machi 28, mwaka huu, yaliyochukua majuma mawili kuanzia Machi 15
hadi 28 mwaka huu Mjini Kibaha.
Akizungumza baada ya kuhitimu
mafunzo Mrashan alisema huo ni mwanzo mzuri katika kuinua mchezo wa riadha
nchini Tanzania.
Chama cha Riadha nchini kimetoa
shukrani zake za dhati kwa Holili Youth Athletics Club (HYAC) kuwa mbele katika
kuinua mchezo wa riadha hasa ikizingatiwa kuwa Nelson Mrashan ni Operation
Manager wa klabu hiyo.
RT kupitia barua yake kwa HYAC
ya Machi 28 mwaka huu ilisema wahitmu wa mafunzo hayo wanapaswa kupewa
kipaumbele katika kutambuliwa kwao ili waweze kutoa taaluma waliyoipata na sio
kukaa na vyeti bila kuwajibika
WAHITIMU
WA MAFUNZO YA UKOCHA MJINI KIBAHA MACHI 28, 2014
|
Haya makocha hao tumewafundisha na wako tayari kufanya kazi yao.
ReplyDeleteSasa kwa nini tuajiri makocha kutoka nchi za nje na makocha wetu wapo ??