HYAC

Attack with Style, Defend with Heart

Tuesday, 18 March 2014

RAIS KIKWETE MGENI RASMI SOKOINE MINI MARATHON 2014



Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika msimu wa pili wa mbio za Sokoine zitakazofanyika katika Kijiji cha Monduli Juu, wilaya ya Monduli, mkoani Manyara, kama sehemu ya maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 30 ya kifo cha aliyekuwa Waziri mkuu wa Tanzania, hayati Edward Moringe Sokoine.
Rais Kikwete anatarajiwa kuwasili wilayani Monduli ambapo pia atahudhuria ibada maalum ya kumbukumbu itakayofanyika katioka kanisa la Monduli Juu na baadae kushuhudia mbio zitakazofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Monduli Juu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mratibu wa Mbio hizo, Wilhelm Gidabuday alisema maandalizi yam bio hizo zitakazofanyika April 12, tayari yameshaanza na kuongeza kuwa kila kitu kinakwenbda sawa kama ilivyokuwa imepangwa.
“Mgeni Rasmi mwaka huu ni Rais Kikwete, tumeshafanya mawasiliano yote na tunaamini mwaka mbio zitafana na kubeba sura ya Utaifa, mwaka jana tulimwalika Rais lakini kutokana na majukumu alishindwa kuhudhuria, lengo letu ni kuhamasisha umoja na uzalendo na sio njaa,” alisema Gidabuda. 
Gidabuday alisema yake imeamua kumwalika kiongozi huyo mkuu wan chi kutokana na Heshimaaliyonayo Marehemu Sokoine katika historia ya Taifa hili na kuongeza kuwa lengo la kuandaa mbio hizo kama ilivyokuwa mwakja jana ni kumbapo pia kutakuwa na watu na viongozi mbalimbali.
Gidabuday alisema kutokana na changamoto  zilizojitokeza mwaka jana, kamati8 yake imejipanga vyema kuhakikisha mbio hizo zinakuwa moja ya mashindano makubwa yanayoandaliwa katika ardhi ya Tanzania ukiacha mbio za Kilimanjaro Marathon zilizofanyika hivi karibuni mjini Moshi.
“Tumejiweka sawa, mbio za mwaka jana zilituachia mengi ya kujifunza na kwa mwaka huu tunaamini tumejifunza na tuko tayari kuwapa Watanzania burudani ya kweli, niseme tu kwamba mwaka huu tumelenga kufanya mabadiliko makubwa sana ukianza na zawadi kwa washindi,” alisema Gidabuday.
Aidha Gidabuday alisema zaidi ya wanariadha pamoja na watu mbalimbali mashuhuri wakiwemo wabunge na Viongozi mbalimbali wakuu wa nchi tayari wameshajitokeza na kuthibitisha kushiriki mbio hizi ambazo lenge lake ni kuhamasisha uzalendo na mshikamano.
Baadhi ya waliomba mpaka sasa ni wanafuzni wapatao 200 kutoka katika shule za msingi na Secondari katika maeneo ya jirani na Kijiji cha Monduli Juu mbio zitakapofanyikia, wanariadha wazoefu akiwemo mshindiu wa mwaka jana kilomita 21, Dickson Marwa kutoka Klabu ya Riadha ya Holili, Holili Youth Athletic Club (HYAC).
Gidabuday aliwataja wengine kuwa ni pamoja na watu wazima ambao mpaka sasa wameshafikia 50 ambapo  kwa mwako huu jumla ya washiriki zaidi ya 1000 wanatarajiwa kushiriki.

Imeandikwa na Fadhil Athuman, Monduli-Arusha

No comments:

Post a Comment