Holili Youth Athletics Club (HYAC)
ya mkoani Kilimanjaro imepata ugeni kutoka Afrika Kusini huku ikiajiandaa na
ushiriki wake Kili Marathon 2014.
DEBBIE
HARRISON, DOMICIAN GENANDI NA PAUL RAILTON
|
Ugeni kutoka nchini Afrika Kusini
umeongozwa na Deborah Harrison mwandaaji wa Kili Marathonmbio zilizo kivutio
nchini Tanzania.
DOMICIAN
GENANDI AKITOA MAELEZO KWA WAGENI KUTOKA AFRIKA KUSINI
|
Debbie Harrison kama ambavyo
amekuwa akitumia aliwasili katika Ofisi za HYAC mjini Holili, mpaka mwa
Tanzania na Kenya majira ya saa 5:20 asubuhi akiwa na Mpiga Picha kutoka
SuperSport Paul Railton na kupokewa na Mkurugenzi Mtendaji wa klabu hiyo ya
riadha Domician R. Genandi .
Debbie alisema amekuwa
akiratibu mbio za Kili Marathon kwa muda mrefu sasa lakini hakuwa amewahi
kusikia kama kuna klabu ya riadha mkoani Kilimanjaro yenye kambi yake Tarakea wilayani
Rombo.
Aliongeza kusema kitendo
kilichofanywa na HYAC ni cha kuigwa nchini Tanzania kwa ajili ya kuinua riadha
kwa ujumla wake.
Pia alisema kuwaweka kambi
wachezaji wa riadha zaidi ya 15 ni la uzalendo zaidi kutokana na ukweli kwamba
miaka ya nyuma Tanzania ilikuwa juu sana katika riadha.
Ujumbe huo kutoka Afrika Kusini
ulitoka mjini Holili na kuelekea Tarakea kujionea Kambi ya wachezaji HYAC.
KUTOKA
KUSHOTO OPERATION MANAGER NELSON MLASHANI, CEO DOMICIAN GENANDI, PRO JOHNSONJABIR, SUPERSPORT CORRESPONDENT PAUL RAILTON NA DEBBIE HARRISON; MSTARI WA
MBELE WINFRIDA GENANDI, KUKUGONZA
GENANDI, KAREN GENANDI NA HYAC SECRETARY INNOCENT THOMAS
|
No comments:
Post a Comment