HYAC

Attack with Style, Defend with Heart

Tuesday 9 December 2014

KUMRADHI FABIAN JOSEPH, FAMILIA YA RIADHA



 MKURUGENZI WA HYAC, DOMICIAN GENANDI



Klabu ya Holili Youth Athletics (HYAC) inaomba radhi kwa Fabian Joseph mwanariadha aliyeshinda mbio za Uhuru Marathon 2014 zilizofanyika Jijini Dar es Salaam Desemba 7 mwaka huu, kwa kitendo cha mchezaji wetu Deo Lazaro kumtendea visivyo, Deo Lazaro alimng'ata kidole chake kutokana na sababu ambazo mpaka sasa tunaendelea kuzifanyia utafiti, licha ya wawili hao kutuhumiana kwa masuala ya ushirikina. 

Tunaiomba radhi familia yote ya wanariadha nchini na wadau wa michezo kwa ujumla wake kwa tukio hilo, pia mwaandaji wa mbio hizo mwaka huu kwa usumbufu uliojitokeza.
Tutalifanyia kazi suala hilo.

TUNAOMBA RADHI KWA USUMBUFU ULIOJITOKEZA KATIKA TUKIO HILO LA KUSIKITISHA.

Mkurugenzi
DOMICIAN GENANDI
HYAC.

ILIYOPITA

No comments:

Post a Comment