Wanariadha Ismail Juma na
Jackline Sakilu wametwaa taji la mbio za kihistoria za “Bagamayo Half Marathon
2014” zilizofanyika mjini Bagamoyo mwishoni mwa juma.
Ismail Juma (Arusha) na
Jackline Sakilu (JWTZ-Arusha) walitwaa taji hilo wakikimbia kilometa 21 kwa
muda wa saa 1:03.20; 1:06.53 kila mmoja.
Kwa wanaume, Dickson Marwa
alishika nafasi ya pili akikimbia kwa muda wa saa 1:03.27 huku Elia Daudi
kutoka Dodoma akishika nafasi ya tatu akitumia muda wa saa 1:03.58.
Kwa wanawake, Failuna Abdi
(Arusha) alishika nafasi ya pili akitumia muda wa saa 1:12.26, nafasi ya tatu
ikishikwa na Zakia Mrisho (Arusha) akikimbia kwa muda wa saa 1:13.07.
Kwa upande wao Holili Youth
Athletics Club (HYAC) katika mbio hizo za kilometa 21 kwa wanawake mwanadada pekee aliyekimbia mbio
hizo Furaha Sambeke alishika nafasi ya 7 akikimbia kwa muda wa saa 1:20.40
akimpita Banuelia Brighton aliyeshika nafasi ya 8 akitumia muda wa saa 1:26.03.
Kwa wanaume kutoka HYAC, Pascal
Mombo alishika nafasi ya 4 akitumia muda wa saa 1:04.10, wengine ni Nyangero
Patrick (1:04.48), Oswald Kahuruzi (1:05.07), Nelson Priva (1:05.38).
Katika Bagamoyo Historical
Marathon 2014, mbio za kilometa 10 zilifanyika ambapo Joseph Sule (Jeshi la
Magereza-Arusha) alishika nafasi ya kwanza akitumia muda wa dakika 30:37
akifuatiwa na Elibariki Buko (HYAC) aliyekimbia kwa muda wa dakika 30:41
Nafasi ya tatu katika mbio hizo
ilichukuliwa na Msanduki Mohammed (Arusha) akitumia muda wa dakika 30:45,
Godfrey Peter (HYAC) alishika nafasi ya 5 akikimbia kwa muda wa dakika 30:50.
Kwa upande wa wanawake Celina
Amosi (Arusha) alishika nafasi ya kwanza akitumia muda wa dakika 34:16.03,
akifuatiwa na Grace Jackson (Bagamoyo) akikimbia kwa dakika 36:20.13 na nafasi
ya tatu akichukua Irene Chima (HYAC) kwa muda dakika 40:20.13
Mgeni rasmi wa mbio hizo
Mkurugenzi Msaidizi wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Juliana Yassoda
aliwataka wadau kujitokeza kwa wingi kudhamini mchezo huo katika maeneo
mbalimbali nchini, na sio kujikita mjini kwani serikali ipo bega kwa bega na
watanzania kuufanya mchezo wa riadha kurudi katika hadhi yake.
Aidha Dominic Mosha ambaye ni
Mratibu wa Bagamoyo Historical Marathon 2014 aliwapongeza washiriki wa mbio
hizo walivyojitokeza kwa wingi na kuwataka mwaka ujao kujitokeza kwa wingi
kutetea rekodi zao.
Wanariadha wapatao 400
walishiriki kwa mara ya kwanza katika mbio hizo ambazo zitakuwa zikifanyika
kila Jumapili ya kwanza ya mwezi Julai kila mwaka katika mji wa kihistoria wa
Bagamoyo.
PREVIOUS STORY
No comments:
Post a Comment