Suleiman Nyambui
Personal information
|
||||||||||||||||
Born
|
February 13, 1953
Majita Musoma, Tanzania |
|||||||||||||||
Sport
|
||||||||||||||||
Country
|
||||||||||||||||
Sport
|
||||||||||||||||
Event(s)
|
||||||||||||||||
College team
|
||||||||||||||||
Achievements and
titles
|
||||||||||||||||
Personal best(s)
|
1500
metres:
3:35.8[1]
Mile: 3:51.94[1] Indoor 2-mile: 8:17.9[1] 5000 metres: 13:12.29[1] 10,000 metres: 27:51.73[1] Marathon: 2:09:52[1] |
|||||||||||||||
Medal record[hide]
|
Suleiman
Nyambui alizaliwa Februari Mosi, 1953 Majita, Musoma nchini Tanzania.
Huyu ni
mwanariadha nchini Tanzania ambaye alijikita katika mbio fupi na ndefu katika
maisha yake ya riadha. Kwa sasa ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha nchini
Tanzania (AFT).
Alitwaa
Medali ya Shaba katika All Africa Games 1978, medali ya Fedha katika Mbio za
Mita 5000 kwenye Michuano ya Olimpiki 1980 na alishika nafasi ya kwanza katika
marathon kwa miaka 3 mfululizo kati ya mwaka 1987 na 1988. Na ana rekodi nyingi
katika mashindano ya ndani ya nchi.
Nyambui na Riadha
Nyambui
aliachwa mpweke baada ya kumaliza elimu ya msingi, hivyo akaanza kuwa mvuvi
katika wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza.
Alipokuwa Mwanza alipata kuonekana kuwa
ana kipaji cha kukimbia ndipo Chama cha Riadha cha Mkoa wa Mwanza kilipompa
mafunzo na vifaa ambavyo vilimwezesha
kupanda hadi kufikia medani ya kimataifa.
Alijiunga na
Jeshi la Kujenga Taifa na baadaye akiwa mwalimu katika Shule ya Bukumbi iliyoko
kilometa 20 kutoka Jijini Mwanza alipata nafasi ya kwenda kusoma nchini
Marekani ambako alisomea Shahada na Uzamili katika Chuo Kikuu cha Texas, El
Paso (UTEP).
Aliwahi
kupata nafasi ya kufundisha wanariadha wa nchini Saudi Arabia kwa mkataba na
baadaye aliamua kurudi nyumbani Tanzania.
Akiwa nchini
Marekani
Nyambui
alikuwa akisoma nchini Marekani kati ya mwaka 1978 hadi 1982. UTEP alihitimu
akiwa na umri wa miaka 29, akiwa na mataji 4 ya NCAA katika mbio za mita 10,000
akiweka rekodi ya kuwa mwanariadha wa kwanza
katika watano wa daraja la 1 kwa wanaume kupata mataji manne mfululizo.
Pia alishinda
mataji 3 mfululizo ya NCAA ya mita 5,000 akiwa UTEP na alikuwa Bingwa wa Mbio
za Nyika NCAA 1980.
Kubwa zaidi
lililovutia ni katika Michuano ya Millrose (Millrose Games) Jijini New York
Februari 1981, Suleiman Nyambui alivunja rekodi ya dunia ya mita 5000,
akikimbia kwa dakika 13:20.4 akimwaacha Alberto Salazar ambaye alivunja rekodi
ya mita 5000 kwa nchini Marekani.
Baada ya Masomo UTEP
Nyambui
aliiwakilisha Tanzania katika Michezo ya Olimpiki kwa wanaume mita 5,000 mwaka
1980 ambapo, alimaliza wa pili akitanguliwa na Miruts Yifter.
Baada ya hapo
alikimbia mbio fupi na baadaye akatuama katika mbio ndefu.
Alishinda
mara mbili mfululizo Berlin Marathon Oktoba 4, 1987 akitumia muda wa saa
2:11:11; Oktoba 9, 1988 alishinda mbio hizo akikimbia kwa saa 2:11:45 pia mwaka
1988 alitwaa taji la Stockholm Marathon
ILIYOPITA
BOFYA KIUNGO HIKI
Imetayarishwa na:
Jabir Johnson, Afisa Habari na Mawasiliano
Holili Youth Athletics Club (HYAC)
Mei 2014.
No comments:
Post a Comment